Dkt. Shaban Tozzo, mratibu wa shughuli ya Sherehe ya Maadhimisho ya siku ya Punda Duniani yaliyofanyika Kitaifa katika kijiji cha Chambalo, Wilaya ya Chemba, Mkoani Dodoma akimtibu Kidonda Punda ikiwa ni mmoja wapo ya shughuli zilizofanyika katika siku hiyo, kushoto ni Dkt. Charles Bukula Mtaalamu wa Mifugo kutoka INADES-Formation Tanzania
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Abdul Mhinte akimkabidhi cheti Mkurugenzi wa shirila la INADES-Formation Tanzania Mbarawa Kivuyo kwaniaba ya shirika hilo wakati wa maadhimisho ya siku ya Punda Duniani. Cheti hicho ni ishara ya kutambua ushiriki wa INADES- Formation Tanzania kwa kumlinda na kumtetea mnyama Punda na kuhakikisha anakua na haki kama wanyama wengine. Hafla ya Maadhimisho hayo imefanyika katika Kijiji cha Chambalo, Kata ya Chambalo wilayani Chemba, mkoani Dodoma Mei 17,2025
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Abdul Mhinte akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kitabu cha Punda ‘Punda Wangu Maisha Yangu’ kilichoandikwa na shirika la INADES-Formation Tanzania wakati wa maadhimisho ya siku ya Punda Duniani. Hafla ya Maadhimisho hayo imefanyika katika Kijiji cha Chambalo, Kata ya Chambalo wilayani Chemba, mkoani Dodoma Mei 17,2025.