Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Taifa Ndg. Mohammed Ali Kawaida (MCC) amekagua Mradi wa Maji Miji Wilaya ya Mpanda, Mkoa Katavi wenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 22.9.
Mradi hui unatarajiwa kuzalisha Lita milioni 12 za maji kwa siku huku ukilenga kuwanufaisha wakazi wote wa Manispaa ya Mpanda na maeneo jirani waliokuwa wakipata adha kubwa ya upatikanaji wa huduma ya Maji.
Mradi huu umeanza kutekelezwa kuanzia Aprili, 2023 na unatarajiwa kukamilika Oktoba, 2025.