Na Mwandishi Wetu – Addis Ababa, Ethiopia
Tanzania imeshiriki Maadhimisho ya Miaka 25 ya Jumuiya ya Tathmini Afrika (AfrEA) yanayofanyika kwa siku tatu kuanzia tarehe 16 hadi 18 Juni, 2025, katika Kituo cha Mikutano cha Umoja wa Mataifa (UNECA), jijini Addis Ababa, Ethiopia.
![]() |
Ujumbe wa Tanzania umeongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya Ufuatiliaji na Tathmini, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Bi. Sakina Mwinyimkuu.
Washiriki wengine kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu ni Mkurugenzi wa Mipango na Bajeti Bw. Eleuter Kihwele na Mkaguzi Mkuu wa Ndani katika Ofisi hiyo Bw. Exavery Salira.
Maadhimisho hayo ya siku tatu yameandaliwa kwa lengo la kuenzi mchango wa tathmini katika maendeleo barani Afrika, na kuimarisha uwajibikaji wa sera kwa kutumia ushahidi (Evidence Based) katika kufanya maamuzi.
Aidha Washiriki kutoka nchi mbalimbali ndani na nje ya bara la Afrika wanajadili mbinu bunifu na jumuishi za tathmini kwa maendeleo endelevu yenye muktadha wa Kiafrika.
MWISHO