

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameongoza kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (CC) kilichofanyika leo Agosti 21, 2025, jijini Dodoma.
Kikao hicho kimekaa kwa ajili ya kufanya uteuzi wa wagombea Ubunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wabunge wa Viti Maalum, Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar pamoja na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Viti Maalum.
Kikao hiki ni sehemu ya mchakato wa ndani wa chama kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2025, ambapo CCM inaendelea na taratibu zake za kidemokrasia kuhakikisha uteuzi wa wagombea wake kwa ngazi mbalimbali za uongozi.