Simba SC, imethibitisha kukamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji Neo Maema akitokea Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.
Maema amesaini mkataba wa mwaka mmoja wenye kipengele cha kuongeza mwaka mwingine, na anatarajiwa kuongeza ubunifu na nguvu mpya katika safu ya ushambuliaji ya wekundu wa Msimbazi kuelekea msimu mpya.