Jeshi la Polisi limeshapata taarifa ya picha mjongeo iliyopo kushoto mwa taarifa hii inayosambaa katika mitandao ya kijamii na ufuatiliaji wa haraka na wa kina umeshaanza.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa ambaye ndiyo anasimamia msako na ufuatiliaji huo atatoa taarifa kamili muda si mrefu.
Jeshi la Polisi Tanzania linatoa shukrani kwa wote wanaoendelea kutupa taarifa zitakazosaidia na zinazoendelea kutusaidia katika uchunguzi wa tukio hilo.