NA VICTOR MASANGU,KIBAMBA
Mgombea mteule wa nafasi ya udiwani kata ya Kibamba kupitia tiketi ya Chama cha mapinduzi (CCM) Otaigo Mwita ameahidi kuboresha sekta ya afya,elimu na huduma ya maji endapo akipata ridhaa ya kuchaguliwa katika uchaguzi mkuuu wa mwaka 2025.
Kauli hiyo ameitoa wakati wa ufunguzi rasmi wa kampeni za uchaguzi ngazi ya Kata ya Kibamba ambapo amesema kwamba lengo lake kubwa ni kuleta chacha ya maendeleo katika nyanja mbali mbali.
Pia Otaigo amebainisha kwamba endapo akichaguliwa ataweka mipango madhubuti ya kutatua kero kubwa ya upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi wa Kibamba.
“Lengo langu kubwa la kuwania nafasi hii ni kwa ajili ya kuweza kushirikiana na serikali katika kuwaletea wananchi wa Kibamba maendeleo mbali mbali ikiwemo suala la maji.afya,miundombinu ya barabara,pamoja na huduma za kijamii,”amebainisha Otaigo.
Kwa upande wake mgombea Ubunge mteule wa Jimbo la Kibamba kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi (CCM) Angella Kairuki pindi atakapochaguliwa atahakikisha anaboresha miundombinu ya barabara za mitaa ili ziweze kupitika kwa urahisi.
Kairuki ambaye ndiye aliyekuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa kampeni hizo amesema lengo lake kubwa ni kutatua kero na changamoto mbali mbali za wananchi katika nyanja mbali mbali.
“Wananchi wa Kibamba naomba sana mnichague na kunipa kura nyingi ili niweze kuwatumikia katika nyanja mbali mbali ikiwemo suala la maji,miundombinu ya barabara pamoja na kuboresha huduma ya afya pamoja na mahitaji mengjne ya msingi,”amesema Mgombea Kairuki.
Uzinduzi wa kampeni za chama chama cha mapinduzi (CCM) ngazi ya kata ulihudhuliwa na viongozi mbali mbali wa chama,serikali pamoja na wananchi ambao walifika kwa ajili ya kusikiliza sera za wagombea mgombea udiwani pamona na Ubunge.