NA DENIS MLOWE , IRINGA
MJUMBE wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Salim Abri ‘Asas’ ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi Oktoba 29 kupiga kura na kuwachagua viongozi wanaotokana na Chama Cha Mapinduzi.
Salim Abri ambaye pia ni Mratibu wa Uchaguzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini inayoundwa na mikoa ya Mbeya, Iringa, Njombe, Ruvuma na Rukwa ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa kampeni katika jimbo la Kilolo uliofanyika Ruaha Mbuyuni llnalogombewa na Dr. Ritta Kabati.
Salim Abri Asas alisema kuwa kuna kila sababu ya msingi kwa wananchi kuendelea kuwa na imani ya chama hicho kutokana na utekelezaji mzuri wa Ilani katika jimbo hilo.
Alisema kuwa serikali ya awamu ya sita imetekeleza miradi mikubwa ndani ya jimbo hilo na na Wanakilolo ni mashahidi tosha wa miradi ya maendeleo iliyofanyika kwa kipindi kifupi chini ya Rais Samia Suluhu Hassan.
Alisema kuwa kutokana na hilo kura zenu ziende kwa wagombea wa CCM ili kuendeleza pale ambapo waliishia ili kuharakisha maendeleo ya wananchi katika jimbo la Kilolo.
Alisema kuwa ifike wakati wananchi waambiwe ukweli nini walichofanya kwa miaka mitano iliyopita na kitu gani kitaenda kufanywa miaka 5 inayokuja kwa kuwapa kura wagombea ubunge na udiwani wa CCM.
Aliongeza kuwa sababu kubwa na kujivunia ni miradi mbalimbali ya afya ikiwemo vituo vitano vya afya na zahanati 10 vimeweza kujengwa ndani ya mfupi katika jimbo la Kilolo hali ambayo imefanya wananchi wapate huduma za afya kwa wakati.
Vilevile alisema kuwa kwa upande wa sekta ya elimu CCM imejenga madarasa 495, vyoo 352, na maabara tisa katika shule za sekondari na msingi aidha, shule mpya 20 za msingi na sekondari zimeanzishwa.
Aliongeza kuwa miradi mikubwa ya maji imefanyika katika maeneo ya Ilula, Mlafu na Mahenge, huku ujenzi wa daraja la Ruaha Mbuyuni–Msasa na maegesho ya magari ukiendelea.
Mradi wa ujenzi wa sekondari ya wasichana Lugalo wenye thamani ya Sh bilioni 5, barabara ya Ipogolo–Kilolo yenye thamani ya Sh bilioni 65, pamoja na skimu ya umwagiliaji ya Ruaha Mbuyuni yenye thamani ya Sh bilioni 4, ni miongoni mwa miradi mikubwa inayoshuhudia mageuzi makubwa ya miundombinu katika jimbo hilo.
Abri alisema kuwa kwa kasi hiyo ya maendeleo wananchi wasiotambua hayo wana hulka ya upotoshaji tu kwani hakuna
asiyejua kazi kubwa iliyofanywa na Rais Dk Samia na Serikali ya CCM.
“Miradi ya maji ilula ilafu, Mahenge, miradi mikubwa katika wilaya ya kilolo ujenzi wa sekondari lugalo bilioni 5
Bilioni 65 kujenga barabara ya Ipogolo hadi kilolo na skimu ya umwagiliaji bilioni 4 ujenzi unaendelea ni mengine mengi sababu tosha ya wananchi mtuchagulie rais wabunge na madiwani ” Alisema
Akimnadi Ritha Kabati, Mcc Abri alisema kuwa ana uzoefu wa bunge haendi kushangaa shangaa anajua nini vya kufanya bungeni na siku ya kwanza tu anaanza na Kilolo kuisemea bungeni kwa je ni ubaya gani aliofanya hadi mumnyime kura? Nina imani Rita kabati anatosha.
Kwa upande wake, Ritta Kabati aliwahakikishia wakazi wa Kilolo kuwa yeye si mgeni katika siasa za jimbo hilo kwani amefanya kazi kwa karibu na wabunge watatu waliomtangulia, akijua vyema changamoto zinazolikabili jimbo la Kilolo.
Alisema kuwa anaenda Bungeni akiwa na deni la kuwaletea maendelelo wananchi wa jimbo hilo na aliahidi kufanyia haki Ilani ya CCM na kueleza kuwa barabara zitakuwa kipaumbele chake cha kwanza mara baada ya kuapishwa.