Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) inawaomba wataalamu wa afya nchini kutoka Hospitali za Wilaya, Mikoa na Rufaa kuwatuma wagonjwa wenye matatizo ya mshipa wa damu kifuanikutanuka, kuchanika au vyote kwa pamoja (kwa jina la kitaalamu Ascending Aortic Aneurysm and or Dissection) waje kutibiwa katika kambi maalumu ya uchunguzi na matibabu.
Matibabu hayo yatakayofanyika tarehe 03 hadi 11 Oktoba 2025 yatafanywa na wataalamu wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao kutoka Shirika la Cardiostart International la nchini Marekani.
Matibabu yatakayofanyika katika kambi hii ni ya upasuaji mkubwa wa kufungua kifua na kupandikiza mshipa mkubwa wa damu (Aorta) ambao unashida. Upasuaji huu kwa kitaalamu unajulikana kwa jina la Ascending Aorta Repair (Bentall’s Procedure) or Aortic Arch Replacement.
Aidha tunawaomba wagonjwa wenye matatizo ya mishipa ya damu kutanuka, valvu za moyo, mishipa ya damu ya moyo kuziba (Coronary Artery Disease) wafike katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) iliyopo Upanga jijini Dar es Salaam kwaajili ya kufanyiwa uchunguzi na kupata matibabu.
Kwa taarifa zaidi wasiliana kwa simu namba 0716-696217 Dkt. Alex Joseph, 0742062374 Dkt. Sigfrid Shayo na 0788-308999 Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete.
“Afya ya Moyo Wako ni Jukumu Letu”.