Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Zanzibar, Kazi, Uchumi na Uwekezaji Mhe. Shariff Ali Shariff wakitoka katika Jengo la Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa Jijini New York nchini Marekani mara baada ya kushiriki mikutano mbalimbali.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amekutana na kufanya mazungumzo na Kansela wa Jamhuri ya Austria Mhe. Christian Stocker, mazungumzo yaliyofanyika pembezoni mwa Kikao cha 80 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Jijini New York nchini Marekani.
Mazungumzo hayo yamelenga kuimarisha maeneo mbalimbali ya ushirikiano baina ya Tanzania na Austria.