Na Meleka Kulwa -Dodoma
Hospitali ya Benjamini Mkapa (BMH) Yafanikiwa kuhudumia watoto 1,308 katika siku 14 ya Kambi maalum ya macho kwa watoto wachanga hadi miaka 15.
Hayo yamesemwa na Daktari Bingwa wa magonjwa ya Macho kwa watoto kutoka Hospital ya Benjamini Mkapa Dkt.Amon Mwakakonyole wakati akizungumza na waandishi wa habari hospitalini hapo kuhusu taarifa ya kambi hiyo.
Aidha, Amesema kuwa miongoni mwa magonjwa yaliyobainika ni Alegy ya macho,Kengeza,Mtoto wa jicho na presha ya macho.
Pia, Dkt.Amon amebainisha kuwa tangu kuanza kwa kambi hiyo wamefanikiwa kuhudumia watoto 1308 ambapo Kati ya hao watoto 116 walihitaji kufanyiwa upasuaji.
”Naishukuru Serikali pamoja na uongozi wa Hospitali ya BMH kwa kuimarisha Idara ya Macho kwani kumekuwa na mapinduzi makubwa yanayochangia kuwa na huduma Bora.”Amesema Dkt.Amon.
Kambi hiyo maalum ya magonjwa ya macho iliyofanyika Kwa wiki mbili kuanzia septembe 15 na kuhitimishwa September 30.2025 ambapo huduma zote zimegharamiwa na Serikali.