
Jeshi la Polisi limetoa taarifa kwa umma, likieleza kuwa limeona taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii na ndugu wa Humphrey Polepole zikidai kuwa ametekwa na kwamba tayari limeanza kuzifanyia kazi taarifa hizo ili kupata ukweli.
Taarifa iliyotolewa na Msemaji Mkuu wa Jeshi la Polisi, imeeleza kuwa jeshi hilo bado linaendelea kumsubiri Polepole aripoti katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai ili atoe maelezo kuhusiana na tuhuma mbalimbali alizozitoa kwenye mitandao ya kijamii.