
Mgombea mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Emmanuel John Nchimbi akiwasalimia na kuwahutubia Wananchi wa kata ya Kidoma,Mikumi wakati akielekea kwenye mkutano wake mwingine wa kampeni katika kata ya Mwaya,Kilombero mkoani Morogoro leo Oktoba 18,2025.
Baada ya kuwasalimia Wananchi wa eneo la Mikumi,Dkt. Nchimbi alitumia nafasi hiyo kumuombea kura za ushindi wa kishindo mgombea Urais wa chama hicho,Dkt.Samia Suluhu Hassan pamoja na kumnadi mgombea Ubunge wa Jimbo la Mikumi,Ndugu Dennis Lazaro LONDO pamoja na Madiwani.
Balozi Nchimbi anafikia mkoa wa 25 sasa tangu kuzinduliwa kwa kampeni hizo Agosti 28,2025 jijini Dar es Salaam,akiendelea kusaka kura za ushindi wa kishindo za mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi,Dkt.Samia Suluhu Hassan,Wabunge na Madiwani.