NA DENIS MLOWE, IRINGA
MKUU wa Mkoa wa Iringa, Kheri James amewataka wajasiriamali mkoani hapa kujitokeza kwa wingi kuomba mikopo inayotolewa na Halmashauri na shangazwa na wakopaji wachache wakati fedha zilizotengwa kuwa nyingi kuliko wakopaji mkoani hapa.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa jengo litakalotumika kama ofisi za Shirikisho la Umoja wa Machinga,Bajaji, Bodaboda, baba/mama lishe, na daladala mkoa wa Iringa liloko katika Soko la Malimbichi la Mlandege, James aisema kuwa mkurugenzi wa manispaa amefanya kazi nzuri ya kukusanya mapato lakini wakopaji hakuna.
Alisema inashangaza kwa kweli Halmashauri imetenga kiasi cha zaidi ya milioni 7000 ila walioomba mkopo wamepatiwa milioni 280 hivyo kuna zaidi ya milioni 500 ipo tu ndani ya Halmashauri hali ambayo inashangaza au mnataka mkurugenzi abadilishe matumizi?
Aliongeza kuwa serikali ya Mama Samia imejipanga kuwakomboa wajasiriamali wote mkoani hapa kwa kuwapa mikopo vijana, kinamama, walemavu na wazee hivyo wasumbueni maafisa maendeleo y jamii wawape elimu ya kukopa fedha hizo ambazo zimetengwa kwa ajili ya wananchi.
Alisema kuwa katika suala la kukopa hakuna jambo jema kama uaminifu na dawa ya deni ni kulipa hivyo waliopatiwa mkopo huo muhimu kulipa kwa wakati ili wengine waweze kukopeshwa.
Rc Kheri James alimpongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa Iringa, Zaina Mlawa kwa utendaji kazi wake na kuweza kutatua changamoto za mbalimbali za Halmashauri kwa wakati na kufanya vyema katika ukusanyaji wa mapato.
Aidha alitoa onyo kali kwa baadhi ya viongozi wa shirikisho la wamachinga kwa tabia ya kuwatoza fedha wakati wa upangaji wa maeneo ya biashara kwa wale waliohamishwa baada ya soko la Mashine tatu kuungua.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Halmashauri ya manispaa Iringa, Zaina Mlawa alisema kuwa jengo la ofisi hiyo limekamilika kwa asilimia 100 na limetumia zaidi ya milioni 60 na kuwa moja ya jengo la kisasa kujengwa na serikali kwa ajili ya shirikisho la Machinga.
Naye Mkuu wa Sehemu ya Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Iringa, Mwantumu Dossi alisema kuwa kwa mwaka wa fedha 2025/2026 Halmashauri ya Manispaa ya Iringa imefanikiwa kutenga mapato ya ndani kiasi cha Shilingi 793,673,600 kwa ajili kukopeshwa.
Alisema kuwa mapato hayo yametengwa kwa mchanganuo ufuatatal ambapoa Wanawake Tshs. 317,469,440/=, Vijana Tshs. 317,469,440/= na Watu wenye Ulemavu Tshs.158,734,720/=) kwa ajili ya kutoa mikopo kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu.
Mwantumu alisema kuwa kwa kipindi cha robo ya kwanza Halmashauri ya Manispaa ya Iringa imepokea maomb ya mikopo kutoka kwa vikundi 28 (Wanawake 15, Vijana 8 na Watu wenye Ulemavu 5) vyenye thamani ya Tshs 280,481,500/= (Wanawake Tshs 157,823,500/=, Vijana Tsh: 103,818,000/= na Watu wenye Ulemavu Tshs 18,840,000/= na jumla ya watu 121 wanaume 25 na wanawake 96 kutoka kata 15.
Aliongeza kuwa Mchakato wa kupata vikundi 28 ambavyo wamepatiwa hundi ya kiasi cha Tst 280,481,500/= vilitembelewa na kuhakikiwa na kamati ya Huduma za mikopo nje ya Kata, Kamati ya Huduma ya mikopo ngazi ya Halmashauri,Timu ya Menejimenti na kujadiliwa na kamati ya Uhakiki Wilaya. Kuridhiwa kwa vikundi hivi umetokana kukidhi vigezo kama Kanuni na Muongozo wa utoaji wa Mikopo wa vikundi unavyoelekeza.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Shirikisho la Umoja wa Machinga Tanzania (SHIUMA) mkoa wa Iringa, Kessy Ndandu, alitoa shukrani za dhati kwa Mh. Daktari Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuona umuhimu wa kuwajengea ofisi yenye ubora na hadhi.
“Tunashukuru sana na hatuna cha kumlipa zaidi kumuombea Afya njema na kumuahidi ushirikiano siku ya tarehe 29 Oktoba 2025” alisema.
Alisema kuwa wamekusanyika wajasiliamali wadogo kutoka makundi ya Shirikisho la umoja wa machinga Mkoa wa Iringa ambalo lina jumla ya wanachama 9,762 kati yao wanaume ni 4,555 na wanawake ni 5,207 ambapo Shirikisho hili linahusisha makundi .mbalimbali yakiwemo wajasiliamali wadogo, Baba na Mama lishe, wafanyabishara wa masokoni, wachimbaji pamoja na wafugaji wadogo.
Pili umoja wa bodaboda Mkoa wa Iringa ambao una jumla ya wanachama 11,752 kati yao 11,740 ni wanaume na 12 ni wanawake.
Tatu ni umoja wa bajaji Mkoa wa Iringa ambao una jumla ya wanachama 2,600 kati yao wanaume ni 2,593 na wanawake ni 7.
Ndadu alisema kuwa mafanikio ya kuanzishwa kwa umoja wa makundi haya kumeleta manufaa mbalimbali kama ifuatavyo kutambulika katika jamii na Serikali, Kusimamia haki za wajasiliamali wadogo Kuunganishwa na taasisi za kifedha kwa ajili ya kukuza mitai na Kujengewa ofisi ambayo imezinduliwa.