

Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya CCM, Rais Dkt. amesema iwapo Watanzania watamchagua na kumpa ridhaa ya kuendelea kuongoza nchi, Serikali yake itajielekeza katika kuhakikisha Watanzania wanapata makazi bora na ya kisasa kupitia mpango maalum wa ujenzi wa nyumba unaoitwa .
Dkt. Samia ameyasema hayo wakati akizungumza kwenye mkutano wake wa kampeni za Urais uliofanyika katika viwanja vya Kesha, Ilala jijini Dar es Salaam tarehe 22 Oktoba 2025.
Akizungumza mbele ya maelfu ya wananchi waliojitokeza katika viwanja hivyo, Dkt. Samia amesema Tanzania inahitaji takribani nyumba milioni tatu (3) kwa mwaka na Serikali yake anayoiongoza ya awamu ya sita imeweka mkakati madhubuti wa kupunguza pengo hilo kupitia miradi ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).
Dkt. Samia ameyanena haya kwa msisitizo ;
“Kwenye makazi tunajitahidi. Nchi yetu inahitaji nyumba milioni tatu kwa mwaka, na kwa sababu hatukuwa tukipunguza hiyo kasi, sasa tunajielekeza kwa nguvu zote kwenye makazi”
Pia, Amefafanua kuwa mpango wa Samia Housing Scheme unalenga kujenga nyumba 5,000 katika maeneo mbalimbali nchini ambapi kati ya hizo, nyumba 560 zimekamilika eneo la Kawe, nyumba 400 zinaendelea kujengwa Mtoni, huku nyumba 1,000 zikitarajiwa kuanza kujengwa karibuni katika maeneo mengine ikiwemo Urafiki (nyumba 200) na Dodoma (nyumba 800).
Aidha, ndani ya Wilaya ya Ilala, Serikali inaendelea na miradi ya ujenzi wa nyumba za makazi na biashara katika eneo la Kariakoo, ikiwemo miradi 16 ya ubia kati ya wafanyabiashara na Serikali.
“Kama mnavyojua Kariakoo ilipata shida. Tumeunda kamati kuchunguza chanzo cha matatizo hayo, na sasa Shirika letu limejielekeza Kariakoo kuhakikisha ujenzi unaendelea”