MUMBAI: MKONGWE wa filamu za Bollywood, Dharmendra Deol, ameweka wazi upendo wake kwa staa wa filamu za India Shah Rukh Khan, baada ya kuweka picha wakiwa wamepiga pamoja na kueleza kuwa ni kama mwanae.
Tukio hilo lilienea haraka mitandaoni na kuzua maoni ya hisia kutoka kwa mashabiki na mwanawe Dharmendra, Bobby Deol.
Dharmendra alishiriki picha hiyo ya zamani, ikionesha wakati wa furaha kati yake na SRK, ikiaminika kupigwa katika hafla ya utoaji tuzo ambapo maelezo ya picha hiyo, aliandika:
“Hawa wote ni kama wanangu. Namshukuru Mungu kila wakati kwa kunipa bahati hii maishani.”
Maneno hayo ya upendo kutoka kwa Dharmendra kwa Shah Rukh Khan yaliwagusa wengi, yakionesha ukaribu na heshima wanayoshirikiana kama vizazi viwili vya mastaa wa Bollywood.
Bobby Deol, mwana wa Dharmendra na pia muigizaji maarufu, alifurahishwa na ujumbe huo wa upendo.
Baadhi ya mashabiki nao waliandika, “Wanaume wawili wenye mvuto katika picha moja,” huku mwingine akisema, “Dharam na Shah, muunganiko wa kupendeza! Kwa nini hukuwemo kwenye filamu ya ‘Dunki’, bwana?”
Kwa upande wa kazi, Dharmendra anatarajiwa kuonekana katika filamu ya ‘Ikkis’, ambayo ni biopic inayotarajiwa kutolewa Desemba 2025.
Shah Rukh Khan kwa sasa anafanya kazi kwenye filamu ‘King’, atakayoshirikiana na binti yake Suhana Khan, inayotarajiwa kutoka mwaka 2026.
Tukio hili dogo lakini lenye maana kubwa limeonesha tena jinsi Dharmendra anavyothamini uhusiano wake na wasanii vijana kama Shah Rukh Khan, na jinsi familia ya Deol inavyoendelea kudumisha urafiki na upendo ndani ya tasnia ya filamu za India.
The post Dharmendra kurudi upya na mwanae Shah Rukh Khan first appeared on SpotiLEO.



