

WAZIRI MKUU wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, ameshiriki ibada ya Jumapili leo tarehe 11 Januari 2026, katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Mashariki na Pwani (DMP), Usharika wa Azania Front, jijini Dar es Salaam.
Ibada hiyo iliongozwa na Msaidizi wa Askofu wa KKKT DMP, Chediel Lwiza, kwa kushirikiana na Mchungaji Victor Makundi. Katika ibada hiyo, waumini waliendelea kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, viongozi wa kitaifa pamoja na amani na ustawi wa Taifa kwa ujumla.
Ushiriki wa Waziri Mkuu katika ibada hiyo umeonesha umuhimu wa kuimarisha mshikamano wa kiroho, maadili na umoja wa kitaifa katika ujenzi wa Taifa.

LUCY ALIYEENDA UBALOZI wa VATICAN KUMSHTAKI KITIMA na WENZAKE AVAMIWA na KUPIGWA na WASIOJULIKANA…
The post Waziri Mkuu Ashiriki Ibada Ya Jumapili Katika Kanisa La Kkkt Usharika Wa Azania Front appeared first on Global Publishers.





