

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Katavi kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Taska Restituta Mbogo, amechangia mjadala katika Bunge la Kumi na Tatu, Mkutano wa Pili, Kikao cha Nne, kilichofanyika leo Februari 05, 2026.
Katika mchango wake, Mbogo aliibua hoja muhimu akiielekeza kwa Wizara ya Kilimo, akisisitiza umuhimu wa mbegu zinazotumiwa na wakulima kufanyiwa utafiti wa kina ili ziweze kutumika tena katika misimu inayofuata na kutoa mazao mengi bila kuathiri ubora wake.
Aidha, Mbogo aligusia sekta ya utalii nchini kwa kuishauri Serikali kuongeza juhudi na uwekezaji zaidi, akibainisha kuwa sekta hiyo ina mchango mkubwa katika pato la taifa.
The post Taska Mbogo Aibua Hoja Nzito za Kilimo na Utalii Bungeni – Video appeared first on Global Publishers.





