Mchezaji wa kimataifa wa mpira wa miguu, Cristiano Ronaldo alizindua chaneli yake ya YouTube siku ya Jumatano, huku mamilioni ya waliojisajili wakijisajili ndani ya saa chache.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno alipakia video 19 kwenye chaneli yake ya ‘UR Cristiano’ ambayo inaangazia maudhui yake na familia yake.
“The wait is over. My @YouTube channel is finally here! SIUUUbscribe and join me on this new journey,” Ronaldo alipost kwenye chanel yake ya Instagram.
Kwa ukuaji huu, Christiano amevunja rekodi ya kuwa na chanel yenye kasi kubwa zaidi ya ukuaji kwenye mtandao wa YouTube.
Ukiachana na YouTube, mchezaji Christiano pia ana wafuasi milioni 170 kwenye mtandao wa Facebook, milioni 112.6 kwenye mtandao wa X na wafuasi milioni 636 Instagram.