Takribani shilingi Trilioni 1.18 zimetumika kujenga miundombinu ya Afya kwaajili ya kutoa huduma za Afya ya msingi na kununua vifaa na vifaa tiba nchini katika kipindi cha miaka mitatu ya serikali ya awamu ya sita.
Taarifa hiyo imrtolewa bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Zainab Katimba wakati akijibu swali la Mhe. Tumaini Magesa, mbunge wa Jimbo la Busanda mkoa wa Geita aliyehoji ni lini serikali itajenga vituo vya kimkakati vya Afya katika kata ya Rwamgasa na Magenge.
Akijibu swali hilo Mhe. Katimba amesema “Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutambua umuhimu na uhitaji wa kuimarisha huduma za Afya msingi na kwa kusikia vilio vya waheshimiwa wabunge katika majimbo yao katika mwaka wa fedha huu naomba mfahamu na mpokee taarifa wote mtapata fedha kaajili ya kuanza kujenga vituo vya afya vya kimkakati” Zainab Katimba Naibu Waziri OR -TAMISEMI
Source Millard Ayo.