
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amemtangaza Profesa Mohamed Yakub Janabi kama muwakilishi aliyechaguliwa kuiwakilisha Tanzania katika kunyang’anyiro cha kuwa Mkurugenzi kikanda wa Afrika katika Shirika la Afya Duniani (WHO).
Uteuzi wa Profesa Janabi ambaye ni Mkurugenzi mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili tangu Oktoba 2022 kumefuatia kifo cha Mheshimiwa Dkt. Faustine Ndugulile aliyechaguliwa kuwa Mkurugenzi kikanda wa Afrika katika shirika hili na Mbunge wa Kigamboni, kilichotokea usiku wa kuamkia tarehe 27 Novemba, 2024 nchini India alipokuwa akipatiwa matibabu.
Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ametangaza uteuzi huo alipokuwa akiwaapisha viongozi wateule Ikulu Ndogo Zanzibar, tarehe 10 Disemba, 2024. Katika shughuli hiyo, Rais Samia alisema,”Tumeangalia CV nyingi, tukaona yako tunaweza kuipeleka kwenye competition ile ya WHO. tunakutayarisha kwenda huko, wakati ukifika tutakupeleke huko CV yako na tutakuingiza kwenye competition.”