
Na Khadija Kalili, Michuzi TV
TIMU ya Tarafa ya Manerumango ‘Mango’ yenye Maskani yake Manerumango Wilayani Kisarawe wameibua kuwa mabingwa katika fainali ya michuano ya Jafo Cup iiyocheezwa tarehe Februari 9 2025 baada ya kuwatoa timu ya Kisarawe 1-0 kwa njia ya penati.
Kipute hicho kimechezwa kwenye Uwanja wa Manerumango Kisarawe Mkoani Pwani ambapo timu ya Mango katika kipindi cha kwanza dakika ya 12 waliifunga Kisarawe na waliendelea kuongoza hadi walipokwenda mapumziko.
Katika kipindi cha pili cha mtanange huo ndipo timu ya Kisarawe ikasawazisha goli hilo na hadi dakika 90 za mechi hiyokumalizika hakukua na mbabe ndipo ikaamuliwa kupigwe mikwaju mitano kwa kila timu pia wote walitoka suluhu ya 4-4 ikaongezwa tena penati moja kwa kila timu ndipo Mango wakawachapa Kisarawe 1-0 na kuibuka washindi wa Jafo Cup.
Kutokana na ushindi huo Mango wamekabidhiwa Kombe,kitita cha Mil.2 na pikipiki mbili zawadi hizo wamekabidhiwa na Waziri wa Viwanda na Biashara, ambaye pia Mbunge wa Jimbo la Kisarawe Dkt.Selemani Jafo.
Timu ya Kisarawe wameshika nafasi ya pili na wamezawadiwa kitita cha MI.1 na Pikipiki moja .
Mshindi wa tatu ni timu ya Mzenga na wanne ni Kurui.
Mbunge Dkt.Jafo amesema ” Nikiwa Mbunge wa Jimbo la Kisarawe na ndiye niliyeandaa michuano hii nimefarijika sana na mwamko wa vijana na wananchi kwq namna walivyojitokeza kucheza na kuehangilia na hii ni kwa mara ya kwanza ushindani umekuwa mkubwa kila mtu aliyefika uwanjani hapa ni shahidi tumeimarisha udugu na umoja kwa wana Kisarawe” amesema Dkt. Jafo.
Wakati huohuo amewahamasisha wananchi wa Kisarawe kujitokeza kwa wingi kwenye zoezi la kuboresha taarifa zao kwenye Daftari la Kudumu la Mpigakura.
“Ninapenda kuwakumbusha kuwa ni wajibu kwa kila mwananchi kwenda kujitokeza kuboresha taarifa zake kwenye Daftari la Kudumu la Mpigakura ikiwa ni katika kuelelea uchaguzi mkuu wa Rais Wabunge na Madiwani hii ni kwa wote waliotimiza umri wa miaka 18 na zaidi au watakaotimiza umri huo wakati au kabla ya tarehe ya Uchaguzi Mkuu wa 2025 na ambao hawajapoteza sifa kwa mujibu wa sheria “amesema Dkt.Jafo .
Aidha zawadi zingine zimetolewa kwa waamuzi 14 huku kila mmoja amepata kiasi cha .Sh.100,000 waalimu wa timu zilizo ingia fainali wamepewa zawadi ambao ni Mango amepata 80,000 Kisarawe 70 , 000 na Mzenga na Kurui amepata kiasi cha 50,000 kila mmoja.
Michuano ya Jafo ilianza kutimua vumbi Julai 2024 ilichezwa kuanzia ngazi ya vijiji katika Kata 17.