Rais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameridhia malipo ya shilingi Milioni 800.65 kwa wananchi 429 wa Kata ya Mkange wanaopisha ujenzi wa Barabara ya Afrika Mashariki inayojengwa toka Tanga kupita Kata hiyo hadi Makurunge Bagamoyo.
Akizungumza katika mkutano huo na wananchi wa vijiji Vitano vya kata hiyo, Mbunge wa jimbo la Chalinze ambaye pia ni Waziri Wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete ameishukuru serikali kwa kuendelea kutatua kero za wananchi na kumshukuru Mhe. Rais kwa kuridhia fedha hizo zilipwe ili wananchi wapishe ujenzi wa barabara hiyo kwa lengo la kuwaletea maendeleo.
Katika hatua nyingine, ameishukuru serikali kwa matayarisho ya ujenzi wa barabara toka Mandera hadi Saadan ambayo inakwenda kufungua fursa kiuchumi.