Na mwandishi wetu
FEDHA zinazotolewa na Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), zitawezesha kujengwa Kituo Kipya cha Afya ili kurahishisha upatikanaji wa huduma za afya Kwa Wananchi katika Kata ya Mlenge Tarafa ya Pawaga Wilaya ya Iringa mkoani Iringa.
Akiwa Mkoani Iringa katika ziara yake Maalum iliyofanyika Februari 20, 2025, Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Deus Sangu, ametembelea na kukagua Mradi wa Ujenzi wa Kituo hicho cha afya.
Aambapo ameridhishwa na hatua iliyofikiwa katika Utekelezaji wa Mradi huo huku akisema kuwa Serikali imeishaandaa mkakati wa kuongeza Pesa ili kuwezesha Mradi huo kukamilika Kwa wakati.
Akizungumza na wananchi wa Tarafa ya Pawaga, Naibu Waziri Deus Sangu ameeleza kuwa Kwa kipindi cha Uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan zaidi ya Shillingi Trilioni nne zimetolewa na Serikali kuingia katika mfuko wa Maendeleo ya Jamii wa TASAF ili kusaidia Kaya Maskini na kutekeleza Miradi mbalimbali ya Maendeleo
Amesema ikiwemo uboreshaji miundombinu ya Barabara na huduma za kijamii Kwa manufaa ya Wananchi, ambapo Kwa Mkoa wa Iringa kiasi cha Shillingi Bilioni 24 kimetolewa na manufaa yake yameonekana Kwa Wanufaika wa TASAF katika Mkoa huo.