Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Nassor Ahmed Mazrui amesema Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete JKCI imekuwa na mchango mkubwa kwa Serikali katika kuwasaidia wananchi wanaosumbuliwa na maradhi ya moyo nchini.
Ameyasema hayo wakati akizindua mkutano wa Cardiotan 2025 pamoja na mafunzo ya awali ya uokoaji wa maisha katika ukumbi wa mkutano wa Shirika la Bima la Zanzibar (ZIC) Mpirani Wilaya ya Mjini Unguja.
Amesema Taasisi hiyo imepiga hatua kubwa ya mafanikio kupitia Serikali ya awamu ya nane kwani imeweza kuokoa maisha ya watu wengi hapa Zanzibar walikokuwa wakisumbuliwa na maradhi ya aina hiyo.
Aidha amefahamisha kuwa lengo la mafunzo haya ni kuhakikisha kuwa wahudumu wa afya, Wafanyakazi wa Mahoteli pamoja na watoa huduma za jamii kuwajengea uwezo wa kutoa msaada sahihi wa haraka ili kuokoa maisha kwa watalii, wageni mbalimbali pamoja na jamii kwa ujumla pale inapotokea dharura ya kiafya ambapo huduma ya kwanza inahitajika ili kuokoa maisha kwa haraka.
Amesema kuwepo kwa miundombinu bora ya utoaji huduma za dharura nchini kutaimarisha na kukuza uchumi wa nchi yetu kwa kuweza kuingiza idadi kubwa ya Watalii nchini.
Kwa upande wake Dkt. Shamila S. Rwegoshora Daktari Bingwa Magonjwa ya Dharura JKCI amesema mafunzo hayo yataweza kumfanya mtu kuwa tayari kumsaidia mgonjwa aliezima hafla kwa kumpa huduma ya kwanza na kuweza kufanya kazi kwa usalama zaidi.
Hata hivyo ameeleza kuwa kutokana na mafunzo hayo kutaweza kujiamini na kuweza kumsaidia mgeni pindi atakapopata tatizo hilo katika maeneo ya kazi na kupunguza vifo vinavyojitokeza juu ya tatizo hilo.
Vilevile amesema kupatiwa mafunzo hayo kwa watembeza wageni kunaweza kuonekana kuwa salama kwa maeneo yote ya Zanzibaar na kupelekea kuengeza idadi ya watalii hapa nchini.
Nae Dkt. Tatizo Waane Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete JKCI Amesema taasisi hiyo imekua mstari wa mbele katika kutoa huduma bora za Afya hapa nchini kwani imekua kitibu watu kjutoka nchi mbalimbali ikiwemo kongo Malawi Uganda na kupata watalii mbalimbali ambao wanatoka Zanzibar na Arusha kwa shughukli za utalii.
Hata hivyo amesema mkutano huo una lengo la kusogeza karibu huduma za afya kwa wananchi hasa huduma za dharura kwa ugonjwa wa moyo kwani tafiti nyingi zinaonyesha vifo vingi hutokea kutokana na jamii kutokuwa na uwelewa juu ya kumkinga mgonjwa juu ya tatizo hilo.
The post Uzinduzi wa mkutano wa kimataifa wa magonjwa ya moyo na mafunzo ya awali ya uokoaji maisha first appeared on Millard Ayo.