
Rais Dkt. Mwinyi amesema hayo alipolifungua Tamasha la Tuzo za Muziki la Trace Awards kwa mwaka 2025 linalofanyika Hoteli ya The Mora ,Matemwe Mkoa wa Kaskazini Unguja .
Aidha, Rais Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa Sanaa ya Muziki ina nguvu kubwa ya kuiunganisha jamii na nyenzo muhimu ya kuchochea Ukuaji wa Uchumi , Uwekezaji na Ubunifu pamoja na kuibua Vipaji vya Vijana katika Sanaa.
Halikadhalika Rais Dkt.Mwinyi ametoa rai kwa Waandaaji na Washiriki wa Tamasha hilo mbali na Kufurahia Muziki bali pia litumike kujenga Ushirikiano, Umoja na Mahusiano mazuri miongoni mwa Wasanii
Ameupongeza Uongozi wa Taasisi ya Trace Award kwa kuamua Tamasha hilo kufanyika Zanzibar kwa mara ya Kwanza kwani litaitangaza Zanzibar Kimataifa pamoja na Kukuza Utalii na kubainisha fursa za Uwekezaji na Utamaduni.