Na Mwandishi Wetu
RAIS Dk.Samia Suluhu Hassan huna deni na watu wa Mkoa wa Tanga! Hivyo ndivyo tunaweza kuelezea kutokana na kasi kubwa ya maendeleo iliyofanywa na Rais Samia katika mkoa huo kupitia sekta mbalimbali.
Kasi hiyo ya maendeleo mbali ya kuleta faraja kwa wana Tanga pia imefanikisha kuwaondolewa kwa changamoto ambazo awali wananchi walikuwa wanakabiliana nazo.
Rais Samia ameanza ziara yake ya kikazi katika Mkoa wa Tanga ambapo pamoja na mambo mengine amekuwa akiifuatilia miradi ya maendeleo na kama inavyofahamika Serikali anayoingoza imetoa Sh.Trilion 3 .1 kwa ajili ya miradi ya maendeleo.
Miradi hiyo ambayo iko katika nyanja mbalimbali imekuwa mkombozi mkubwa kwa wananchi na hivyo kuchochea ukuaji wa maendeleo kwa wananchi mmoja mmoja,wilaya na mkoa kwa ujumla.
Kila wilaya alipokuwa akipita Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kutokana na kasi ya maendeleo yaliyowafikia wananchi wamekuwa wakimlaki wakiwa wamejipanga pembezoni mwa barabara alizokuwa akipita kuelekea kwenye maeneo ya miradi.Ishara ya kumshangalia imetawala katika kila kona.Tasabu la Wananchi wa Tanga linaonekana dhahiri kwa Rais Samia.
Akiwa Mkata katika siku yake ya kwanza ya ziara yake Rais Samia alishuhudia mapokezi makubwa kutokana na wananchi wengi kuwa na shauku ya kumuona na kumsikiliza.Akiwa mbele ya wananchi hao Rais amethibitisha alivyo kipenzi cha Watanzania.
Akizungumza akiwa eneo la Mkata Rais Dkt Samia mara baada ya kufungua Hospitali ya wilaya ya Handeni anawapa mshangao na furaha kubwa wananchi wa mji huo baada ya kutangaza kwamba Hospitali hiyo iwe maalumu kwa ajili ya utoaji wa huduma za matibabu ya mifupa pamoja na magonjwa mengine.
Kauli ya Mkuu huyo wa nchi imekuwa ni faraja na kuwafuta machozi wananchi wa eneo hilo pamoja na wasafiri kutokana na kwamba barabara ya Handeni eneo la Mkata imekuwa ni kiunganishi cha Mkoa wa Tanga na Pwani.
Kutokana na kuwa kiunganishi hicho na wingi wa mabasi,malori pamoja na magari madogo ambayo yanatumia barabara hiyo uwezekano wa kupatikana ajali ni kubwa na hivyo uwepo wa Hospitali hiyo maalumu kwa tiba za mifupa utakuwa ni mkombozi kwa watanzania.
Katika kutilia mkazi jambo hilo,Rais Dkt Samia Suluhu anamuagiza Waziri wa Tamisemi Mohamed Mchengerwa kupelekea kiasi cha milioni 240 kwa ajili ya maboresho zaidi ya kitengo hicho ili iweze kutoa huduma za matibabu hayo.
“Nielekeze Hospitali hii iwe maalumu kwa ajili ya watu wenye matatizo ya mifupa na menginevyo nah ii itasaidia sana …lakini niwaambieni ujenzi wa Hospitali hii umekuwa ni wa viwango vikubwa kama mkoa.
“Hivyo nimuagize Waziri Mohamed Mchengerwa iwe inatoa tiba ya mifupa kutokana eneo hili kuwa lipo barabarani ambapo kuna uwezekano wa uwepo wa ajali lakini na huduma hizi za kibingwa haziwezi kupatikana kila mahali.”
Hatua hiyo ya Maelekezo hayo ya Mkuu wa Nchi ikiwaibua wananchi ambao walieleza namna ambavyo wamefurahishwa na hatua hiyo .
Akizungumza katika mkutano huo Bakari Juma ambaye ni mkazi wa Mkata anasema wamefurahishwa na utendaji kazi wa Rais kutokana na kugusa maeneo yote muhimu ikiwemo afya,elimu na huduma nyengine za kijamii
“Rais anafanya kazi kubwa na nzuri kwa sababu kipindi cha nyuma wakina mama walikuwa wanalala porini kwa ajili ya kutafuta huduma ya maji lakini kwa sasa wanaipata kwa hatua tano tu.Kwa kweli katika hili nimshukuru sana Rais Dkt Samia kwa kutuletea huduma ya maji kutokana na kwamba maji kwetu hapa yalikuwa ni kilio kikubwa lakini kwa sasa kimekwisha.”
Mkazi mwingine wa eneo hilo Asia Rajabu anasema wanamshukuru Rais Dk.Samia kutokana na kazi kubwa ya kuboresha shule pamoja na elimu bure ambayo imekuwa mkombozi mkubwa kwa watoto wao.
Kwa upande wake Athumani Lawi anasema wilaya hiyo ilikuwa na shida kubwa ya maji safi lakini kwa sasa maji wanayapata kila wakati na hivyo wanamshukuru Rais kwa kuwaepusha na changamoto hiyo muhimu.
“Nilitamani nimshike mkono ila napenda kumwambia Rais wangu hongera kwa kazi kubwa na nzuri na sisi tunamuhaidi mama mitano tena na niwaambie wapinzani hawana nafasi,”anasema.
Akiwa kwenye ziara yake wilayani Lushoto na Korogwe, Rais Dkt Samia alifungua Jengo la Halmashauri ya Bumbuli lenye vyumba 72 ambalo Serikali yake ilitoa Sh.Bilioni sita kwa ajili ya ujenzi ambao umekamilika kwa asilimia 100.Jengo hilo litatoa mchango mkubwa katika kuboresha huduma kwa wananchi.
Vyumba hivyo vitatumika na watumishi wa Serikali wakiwemo wakuu wa idara za Halmashauri ya Bumbuli hivyo kutoa nafasi nzuri ya kuimarisha utendaji kazi wa Serikali katika kutoa huduma kwa wananchi kwa haraka na ufanisi.
Ujenzi wa miundombinu ya Jengo hilo ni ya kisasa na umezingatia mahitaji ya watu wenye mahitaji maalumu ,Kumbi kubwa na ndogo za mikutano za kisasa zilizopo ambazo zinatoa fursa nzuri kwa viongozi na wananchi kufanya majadiliana na mikutano.
MIRADI YA NISHATI
Akiwa Wilaya za Korogwe na Kilindi wananchi wanampongeza Rais kwa Serikali anayoisimamia kutekeleza miradi ya umeme Vijijini ambapo katika wilaya ya Korogwe vijiji vyote vimefikishiwa huduma hiyo muhimu.
Pongezi za wananchi hao zinatoka kwa Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini Timotheo Mzava ambayo anaeleza Machi 15 mwaka 2021 alikuwa kwenye viwanja hivyo na wao wabunge walipata nafasi ya kutoa maombi yao ikiwemo umeme vijijini,hivyo wanashukuru ametekeleza.
“Vijiji vyote 118 vya Korogwe Vijijini vimefikiwa na nishati ya Umeme na wananchi wanaendelea kujishughulisha na shughuli za kiuchumi zinazotumia umeme.Kuhusu Ujenzi wa Kituo cha kupoza umeme Handeni kuimarisha upatikanaji wa Umeme”
Hata hivyo Rais Samia anasema utekelezaji wa ujenzi wa kituo cha kupokea na kupoza umeme cha Handeni utakapokamilika utaboresha upatikanaji wa umeme katika wilaya za Handeni na Kilindi pamoja na maeneo jirani.
Ameyasema hayo alipokuwa akizundua Shule ya Wasichana ya Kilindi na Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Handeni ambapo anasema tatizo la umeme kwenye wilaya hiyo wanalifahamu na wameanza kuchukua hatua kwa ujenzi wa kituo cha kupoza umeme kitakachogharimu Sh.Bilioni 50,hivyo kitaboresha upatkikanaji wa umeme.
Rais Dkt Samia anasema upatikaji wa Umeme wa uhakika Handeni utasaidia ukuaji wa uchumi pamoja na kuyainua madini ya kinywe ambayo yanapatikana wilayani Kilindi kwani yanahitaji umeme wa kutosha.
Akizungumza kwa niaba ya wananchi wa Jimbo la Kilindi Mbunge wa Jimbo hilo Omari Kigua anaanza kwa kuishukuru Serikali kwa kutoa fedha zaidi ya Bilioni 98 kwa ajili ya kutekeleza mradi wa gridi imara utakaohusisha ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme kutoka Mkata kupitia Handeni hadi Kilindi
Awali akizungumza wakati wa ufunguzi wa Jengo la Hospitali ya wilaya ya Handeni Waziri wa TAMISEMI Mohamed Mchengerwa amemueleza Rais Dkt Samia kuwa wananchi wa Handeni wanamshukuru kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuliunganisha Taifa ikiwemo kuwapeleka wadau ambao waliwashika mkono wakajenga majengo mbalimbali na kuifanya hospitali hiyo kwa bora na yenye viwango vya hospitali ya mkoa.
Mchengerwa anasema ujenzi wa jengo hilo ni mpango wa Serikali kuendelea kusogeza huduma karibu na wananchi na maelekezo ya Rais Dkt Samia Suluhu ya kuelekeza kwamba yajengwe majengo kwa ajili ya kuwahudumia wananchi wa handeni na hiyo ni kazi kubwa ya kuunganisha Taifa na mahusiano na watu mbalimbali duniani.
“Wananchi walipata bahati ya kupata wadau wa maendeleo kutushika mkono na kujenga majengo mbalimbali na kuifanya Hospitali yetu kuwa bora na yenye viwango vya Hospitai ya mkoa na kazi hiyo imekwenda kuokoa maisha ya watoto, wakina mama wanaokwenda kujifungua na maisha ya wapiti njia”Anasema
Hata hivyo anasema kwamba Serikali imewezesha ujenzi wa Majengo 15 ya huduma za maabara, majengo muhimu za huduma za nje, huduma za dharura, huduma za mionzi,jingo la huduma za wuzazi ,jengo la dawa na kipindi cha muda mfupi umweza kuokoa maisha ya wakina mama na watoto.
“Mhe Rais Sekta ya Afya inafanya kazi kubwa ya kuokoa maisha ya wakina mama na watoto na wilaya ya Handeni hakuna kifo cha mama na mtoto na wahudumu katika sekta hii wamebadilika na wanafanya kazi kwa bidii kuhakikisha wanaokoa maisha ya watanzannia.
Hata hivyo alisema katika Mkoa wa Tanga fedha ambazo zilitolewa na Serikali kwenye sekta ya afya wametoa Bilioni 65.6.
Akiwa katika ufunguzi wa Hospitali hiyo Rais Dkt Samia alimtaja Ummy Mwalimu aliyekuwa kwa kumshukuru kutokana na mwamba ndiye aliyeanza ujenzi wa hospitali hiyo na kazi nzuri imefanyika mpaka alipomkabidhi kijiti Waziri wa sasa Jenista Mhagama.
WILAYANI BUMBULI
Akiwa kwenye ziara yake kwenye Halmashauri ya Bumbuli Rais Dkt Samia Suluhu alifungua Jengo la Halmshauri hiyo anasema kwamba alimpiga kofi Mbunge wa Jimbo la Bumbuli January Makamba lakini akamfichia chakula kama ilivyo uhusiano wa mama na mwana.
Akizungumza mbele ya wananchi wa Lushoto, Rais Dkt Samia alimuita mbele ya hadhara na kumkumbatia akieleza kwamba mfano wa kifamilia jinsi alivyosimamia uhusiano wao .
“Lakini mwisho kabisa nataka nimuite mwanangu January hapa aje arudi kwa mama sisi wamama mnatujua, ukimkera mama anakupiga kofi anakufichia chakula sio ndio hivyo sasa mwanangu nilimpiga kofi na kumfichia chakula lakini leo namrudisha kwa mama haya njoo mwanangu “Anasema.
Akielezea namna Serikali ilivyojipanga kukabiliana na wanyama wakali-Rais Dkt Samia anasema wataendelea kubuni mbinu mbalimbali za kubaliana na wanyama pori wakali na waharibifu huku akielekeza wizara ya Maliasili na Utalii kuangalia namna ya kupitia upya kanunua za malipo ya kifuta jasho/machozi.
“Tutaendelea kuongeza askari wanyamapori na kubuni mbinu mbalimbali za kufukuza wanyama wakali na waharibifu ikiwemo kutumia ndege nyuki (Drones)
Akiwa katika wilaya ya Korogwe Mkuu huyo wa nchi anatoa maelekezo kwa Waziri wa Afya Jenista Mhagama kutoa fedha kwa ajili ya ukarabati Hospitali ya wilaya ya Korogwe (Magunga) ili wananchi wapate huduma bora za afya.
“Akizungumza katika uwanja wa Chuo cha Ualimu Korogwe,Rais Dkt Samia anasema kwamba changamoto nyengine zilizotajwa ni ukarabati wa Hospitali na vizuri nipo na Waziri wa Afya juzi tu tulikuwa na mgeni katika maongezi yetu kuna visenti tumevipata naomba umege uleta kwenye Hospitali hii ili vije kufanya ukarabati”
Hata hivyo Rais Dkt Samia ameweka jiwe la Msingi mradi wa Maji wa Miji 28 utakaohudumia miji ya Handeni, Korogwe, Muheza na Pangani.
Akizungumza mara baada ya kuweka jiwe la msingi Rais Dkt Samia anasema wizara hiyo kwa sasa imetoka kuwa wizara ya lawama na kuwa wizara ya mfano huku akiwapongeza kwa kazi nzuri wanayoifanya.
Anasema mwaka 2021 walikuwa wanasukumana sana lakini tokea mwaka 2022 sekta ya maji imekuwa ikifanya vizuri na kazi yake kubwa ni kutafuta fedha wao waendelee na kazi ya utekelezaji.“Niwapongeze watumishi wote wa sekta ya maji na endeleeni kuchapa kazi.”
Pamoja na hayo Rais Samia amesema amefanya kazi kubwa ya kutafuta fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi na amekuwa akitiwa moyo na wizara kutokana na usimamizi mzuri ambao umewezesha mafanikio makubwa katika usimamizi na utekelezaji wa miradi.
Na ndio maana tuna kila sababu ya kusema Rais Dkt Samia Suluhu hauna deni na watu wa Tanga na mitano tena.Wana Tanga tunajua huu ni mwaka wa Uchaguzi Mkuu, kwako Rais Samia tunasema MITANO TENA.Huna deni ila sisi tunadeni lako,tutakulipa kwa kukupigia kura ya ndio. Hongera Rais Samia,Tanga tunakupenda,tunakuthamini.