TAASISI ya Elimu Tanzania (TET)imetoa rai kwa wazazi na walezi wenye watoto wanaosoma madarasa ya awali, msingi, sekondari ,vyuo pamoja na watu wenye mahitaji maalum kununua vitabu vya mitaala mipya vinavyopatikana katika taasisi hiyo na kuuzwa maeneo mbalimbali nchini
Rai hiyo imetolewa Jijini Arusha na Mkuza Mtaala wa TET ,Bi. Zena Amiri wakati akiongea na wananchi wanaoendelea kufika katika banda hilo kwaajili ya kununua vitabu vya mitaala iliyoboreshwa zinavyopatikana kwa bei nafuu ndani ya banda hilo kupitia kampeni mahsusi ijulikanayo kama Kitabu Kimoja ili kufikia uwiano wa kila mwanafunzi .
Amesema taasisi hiyo inajukumu kubwa la kutafsiri sera ya elimu na kuweka kwa vitendo kwa kutengeneza mtaala ulio bora lakini pia taasisi hiyo inakazi kuu nne ikiwemo kufanya tafiti mbalimbali, mtaala wa elimu, vifaa ikiwemo mafunzo elekezi kwa viongozi mbalimbali wa elimu katika makundi mbalimbali ikiwemo wanafunzi, walimu, wazazi na makundi maalum.
“Mitaala iliyoboreshwa inalengo la kutoa elimu nyumbufu ambayo inamfanya mwanafunzi kusoma na kuenda katika taaluma yake husika na katika maonesho haya ya Siku ya Wanawake Dunia yenye kauli mbiu Wanawake na Wasichana 2025 tuimarishe Haki, Usawa na Uwezeshaji”
Naye Bi. Hadija Salumu mhakiki wa vitabu vya maandishi ya breli amesema katika taasisi hiyo wanapigachapa vitabu vya maandishi ya breli kwa shule za msingi, sekondari na vyuo ili kuwasaidia wanafunzi wasioona kusoma maandishi yao hivyo alisisitiza wazazi na walezi kuwapeleka watoto wao shule ili waweze kusoma na kutimiza ndoto zao
Wakati huo Mkuza Mitaala wa somo la kifaransa kutoka TET, Maria Jeremia alisisitiza katika maadhimisho ya wiki ya wanawake taasisi hiyo inahamasisha wananchi kununua vitabu ikiwemo vitabu kwa watoto wasioona ili nao waweze kufikia malengo yao.