Na Humphrey Shao
Wakala wa barara mijini na Vijijini Tarural Mkoa wa Dar es Salaam imekwisha anza kutekeleza miradi mikubwa yanujenzi wa barabara za DMDP awamu ya pili katika Wilaya zote za Ubungo ,Ilala, Kinondoni , Temeke na Kigamboni.
Hayo yamethibitishwa na Meneja Tarura Mkoa Mhandisi Geofrey Mkinga akizungumza wakati wa kikao cha kamati ya ushauri wa barabara cha mkoa wa Dar es Salaam, amesema kuwa utekelezaji wa miradi ya DMDP umekwisha anza na baadhi ya wakandarasi wapo saiti.
” miradi ya DMDP iliyosainiwa imekwisha anza toka tarehe 15 mwezi wa kwanza sasa hivi wakandarasi wote wakosaiti wanafanya kazi za awali za uondoaji miuondombinu ya Tanesco na Dawasa hili mradi ukianza kusiwe na usumbufu” amesema mkinga.
amesema kuwa hatua nyingi za awali za kimikataba zimefika mwisho sasa tumeingia katika utekelezaji hivyo ni jambo la lazima kuondoa miundo mingine hili tuweze kuweka mitambo barabarani.
ametaja pia pamoja na miradi hiyo mikubwa pia kwa sasa wameanza ukarabati wa maeneo ambayo yaliathiriwa na mvua za elnino pamoja na utekelezaji wa miradi midogo midogo