
Na Khadija Kalili, Michuzi TV
KIWANDA Cha Doweicare kilichopo eneo la Lulanzi Picha
yandege Wilayani  Kibaha wametoa  mchango wa fedha ikiwa katika kuchangia  ujenzi wa kalavati.
Mkurugenzi wa Kiwanda hicho Bob Chaing amesema kuwa  wamekabidhi kiasi cha Sh.500,000 kwa Uongozi  wa Serikali ya Mtaa ya Lulanzi  huku  akisisitiza  na kusema kuwa wamekuwa wakishiriki kwenye shughuli mbalimbali  za kijamii Wilayani  hapa na ndani ya Mkoa wa Pwani kwa ujumla.
Doweicare  ambao ni wazalishaji wa taulo za kike (Softcare Sanitary Pads) tunayofuraha kubwa kurejesha kwa jamii japo itaonekana ni kidogo lakini tunayorekodi ya kuchangia huduma  nyingi ” amesema Chaing.
Amesema kuwa wanapokuwa na nguvu wanachangia na hata pindi daraja  litakapokamilika watakuwa sambamba.
Akizungumza  leo  tarehe 5 Februari 2025 Mwenyekiti wa Mtaa wa Lulanzi. Thomas Shilole  amewaeleza  Waandishi wa Habari  kuwa wanashukuru kwa mchango huo kwani  eneo hilo limekuwa korofi  kupitika hasa nyakati za mvua.











