Na Janeth Raphael MichuziTv -Dodoma
MKUU Wa Mkoa Wa Dodoma Rosemary Senyamule Ameagiza Mamlaka zinazohusika na ujenzi wa miundombinu mbalimbali katika Mkoa wa Dodoma kuhakikisha Miradi Isiyokamilika inapewa Kipaumbele Ili iweze Kukamilika Kwa Wakati.
Pamoja na kuhakikisha kwamba barabara zinazounganisha wananchi kupitia Reli ya mwendo kasi kuwa sehemu ya kipaumbele hicho ili wananchi wafurahie mradi huo mkubwa kwani hautakuwa na athali katika shughuli zao za za kila siku.
RC Senyamule Ametoa Maagizo Hayo Leo Jijini Dodoma katika Kikao Cha Bodi Ya Barabara Mkoa Wa Dodoma Ambapo Amesema Wakati Wataalam Wakiendelea Na Mchakato Wa Bajeti Kwa Sasa Vipaumbele Hivyo Viendane Na Vipaumbele Vya Kimkoa.
“Naomba vipaumbele ambavyo tumevisema hapa vipate uzito stahiki kulingana na vipaumbele vya kimkoa ili twende pamoja, moja wapo ni sehemu yenye magonjwa ambayo ndiyo kipaumbele cha kwanza na miradi isiyokamilika ipewe kipaumbele kingine”.
“Pia maeneo ambayo yanatakiwa yawekwe barabara kuunganisha wananchi kupitia Reli ya Mwendokasi lazima yawe ni sehemu ya kipaumbele ili wananchi wafurahie huo mradi mkubwa kwasababu haujawaathiri na wao wana njia za kupita hiyo ikiwa sambana njia zote zinaunganisha Mji”.
Aidha Senyamule amesema kuwa kipo kipaumbele kingine cha kimkoa ambapo wanataka kuimarisha utalii wa Mkungunelo eneo ambalo ni zuri lakini ufikaji wake pale unataka mipango ya barabara ili eneo liweze kufikika kirahisi.
Vile vile amewakunbusha Shirika la Umeme Tanzania Mkoa wa Dodoma kuweka kipaumbele kwenye maeneo ya uwekezaji ambayo wanafikiri kuwa kukamilika kwake kutaendelea kukuza uchumi wa Mkoa wa Dodoma na kuwavutia zaidi Wawekezaji.
Awali akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa kazi za matengenezo dharura na miradi ya maendeleo Zuhura Amani ambaye ni Mkurugenzi wa Tanroads Mkoa wa Dodoma amesema kuwa Tanroads inahudumia jumla ya Barabara zenye urefu wa kilomita 1,707.22 na kati ya hizo 604.29 ni za lami ambazo zinajumuisha barabara kuu na Barabara za Mkoa.
Na kuongeza kuwa hali ya Barabara hizo ni nzuri kwani matengenezo yanaendelea katika Barabara hizi kwa kazi ya mwaka 2024/25.
Na kwa upande wa miradi ya matengenezo amesema hadi sasa jumla ya mikataba 42 imesainiwa yenye thamani ya Shilingi Bilioni 13.5 ikiwa ni sawa na asilimia 81.03.
Naye George Malima ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Mpwapwa ambako kunadhaniwa kuwa na changamoto ya Barabara ameiomba Bodi hiyo kuwaokoa wananchi wa Mpwapwa kwa kujengewa walau Barabara za Mchepuko na Barabara korofi inayotoka Kongwa mpaka Mpwapwa Mjini ili kuendelea kujenga Imani kwa Wananchi hao kwani kwa Taarifa aliyonayo inaonesha kuwa fedha za ujenzi wa Barabara hiyo tayari zimekwisha kutoka Wizara ya Fedha na kwenda Tanroads na iko hatua za mwisho kumlipa Mkandarasi.
Kikao hicho cha Bodi ya Barabara Kimetoka na Maazimio 6 Ikiwa Ni pamoja Mkoa kuunda Tume Ya Wajumbe Wa Bodi Ya Barabara Pamoja Na Wataalam Husika Ili Kufanya Ufuatiliaji Wa Fedha Za Miradi Ya Barabara, Tanroads Kupeleka Taarifa Ya Ujenzi Wa Vivuko Vya SGR Eneo La Mkonze Kabla Au Ifikapo March 18, Vipaumbele Katika Miundombinu Ya Maji Iwe Kumalizia Miradi Ambayo Inaendelea Hususani Visima Vilivyobaki Katika Utekelezaji.