Mkurugenzi Mtendaji wa Mzuri Afrika Shaban akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kuleta mashine za Teknolojia ya Kisasa za kulima,jijini Dar es Salaam.
Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Mzuri World, Marek Rozniak akizungumza kuhusu mashine za Kisasa za Kilimo na Tanzania ni nchi ya pili,jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya Watendaji wa kampuni ya Mzuri Afrika katika picha ya moja.

Baadhi ya Watendaji wa kampuni ya Mzuri Afrika katika picha ya pamoja.
*Mashine mojawapo inalima hekari 10 kwa saa moja
Na Mwandishi Wetu
kampuni ya Mzuri World imeleta mapinduzi kwa kuzindua mashine za kisasa za kulimia, kupanda, na kunyunyizia dawa shambani
Kaampuni hiyo inazalisha mbolea za kimiminika, ikiwa tayari imesajili aina 11 za mbolea nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi Mtendaji wa Mzuri Afrika, Shaban Mgonja, amesema kuwa hatua hii inalenga kuboresha kilimo cha Tanzania kwa kutumia teknolojia za kisasa ambazo zinapunguza gharama za uzalishaji na kuongeza tija kwa wakulima sambasamba na kulinda ardhi.
“Mimi ni Mtanzania, na kwa kutambua kuwa kilimo ni uti wa mgongo wa taifa letu, nimeona ni muhimu kuleta teknolojia itakayosaidia wakulima kuongeza uzalishaji wao kwa ufanisi mkubwa,” alisema Mgonja.
Mashine ya Mzuri si ya kawaida, kwani inachanganya hatua tatu muhimu za kilimo: kulima, kupanda mbegu, na kuweka mbolea kwa wakati mmoja.
Amesema Teknolojia hii imeenea katika nchi 50 pekee duniani, na sasa Tanzania ni moja ya nchi zinazofaidika na utumiaji wa teknolojia.
Mashine hii inapatikana katika ukubwa tofauti, ikiwa na uwezo wa mita 3 na inalima heka 6 kwa saa moja,Mashine ya mita 4 inalima heka 10 kwa saa moja pamoja na Mashine ya mita 6 inalima heka 15 kwa saa moja.
Mgonja amesema kuwa uwezo huu, mashine za Mzuri zinapunguza muda wa kazi, gharama za uendeshaji, na kuhakikisha kilimo kinakuwa cha kisasa na chenye tija zaidi
ili kuhakikisha wakulima wanaelewa vyema manufaa ya mashine hii, Mzuri World imeandaa shamba maalumu lenye ukubwa wa heka 300 lililopo Vigwaza, Kibaha – Pwani, ambako wakulima wanaweza kuona kwa vitendo jinsi teknolojia hii inavyofanya kazi.
Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Mzuri World, Marek Rozniak, amesema kuwa lengo la kampuni hiyo si kuuza mashine tu, bali pia kusaidia wakulima kutumia teknolojia mpya ili kuokoa muda, mbegu, na mbolea huku wakipata mavuno mara dufu.
“Teknolojia ya Mzuri inasaidia wakulima kutumia raslimali zao kwa ufanisi mkubwa. Kwa kutumia mashine hizi, mkulima anaweza kupunguza gharama za uzalishaji huku akiongeza mavuno yake kwa kiwango kikubwa,” alisema Rozniak.
Amesema kwa maendeleo hayo kwa wakulima wa Tanzania sasa wana fursa ya kubadili mfumo wa kilimo kutoka wa jadi kwenda wa kisasa, jambo ambalo litasaidia kuongeza uzalishaji wa chakula na mazao ya biashara kwa tija zaidi.