NA VICTOR MASANGU, KIBAHA
Mke wa Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Mama Selina Koka amewahimiza wanawake kuachana na kuwa na tabia ya kuwa tegemezi na badala yake wahakikishe wanachapa kazi kwa ushirikiano wa pamoja katika shughuli zao mbali mbali za maendeleo kwa lengo la kuweza kujikwamua kiuchumi na kuondokana na wimbi la umasikini.
Mama Koka ameyabainisha hayo alipokuwa mgeni rasmi wakati wakati wa sherehe za maadhimisho ya siku ya mwanamke duniani ambapo ambayo yamefanyika katika ukumbi wa Kibaha shooping Moll na kuhudhuliwa na viongozi mbali mbali wa serikali, viongozi wa vyama, wajasiriamali pamoja na wanawake kutoka makundi tofauti katika Halmashauri ya Kibaha mji.
Amesema kwamba kupitita maaadhimisho hayo wanawake wanapaswa kubadilika na kuwa na kupendana wenyewe kwa wenyewe ikiwa pamoja na kuweza kuchangamkia fursa za mikopo ambayo itaweza kuwasaidia kukuza mitaji yao na kuiendeleza katika suala zima la kufanya biashara zao.
“Nimefarijika sana kushiriki na wanawake wenzangu katika siku hii ya maadhimisho ya siku ya mwanamke dunia lakini kitu kikubwa ninachowaomba mnatakiwa kuwa na ushirikiano na upendo wa pamoja katika mambo mbali mballi ikiwa pamoja na kuchangamkia fursa za mikopo ambayo itaweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa katika kuendeshea biashara zao na hatimaye kujikwamua kiuchumi,”amesema Mama Koka.
Pia amewahimiza wanawake hao kuhakikisha kwamba wanakuwa na malezi bora kwa watoto wao ikiwa pamoja na kuwalinda kwa pamoja bila ya kuwa na ubaguzi wowote na kuwapatia haki zao zote za msingi ikiwemo elimu sambamba na mahitaji mengine yanayostahili.
Katika hatua nyingine amempongeza kwa dhati Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kutenga fedha amabzo zimeweza kusaidia katika kutekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo na kuwaomba wanawake kumpa sapoti ya kutosha katika kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 na kumpa kura nyingi za kishindo.
Kwa upande wake mkuu wa Idara ya maendeleo ya jamiikatika Halmashauri ya mji Kibaha Leah Lwaji amesema kwamba lengo kubwa ni kuwawezesha wanawake katika makundi mbali mbali katika kuwainua katika nyanja ya kiuchumi pamoja na kuwakumbusha umuhimu wa haki, usawa pamoja na uwezeshaji katika kuchochea suala zima la maendeleo endelevu kwa wananchi.
“kupitia maadhimisho haya tunawakumbusha wanawake kuhakikisha umuhimu wa haki saawa pamoja na uwezeshwaji,kwa lengo la kuweza kuchochea ukuaji katika sekta ya uchumi, maendeleo jumuishi na ustawi wa jamii, kwa maendeleo endelevu kwa wanawake, ili waweze kufikia malengo yao.
Aidha amesema kwamba Halmashauri ya Kibaha mji bado inaendelea na uhamasishaji na uelimishaji kwa wananwake juu ya umuhimu wa kondoa mila ambazo zimepitwa na wakati amabpo imefanikiwa kupita na kutoa elimu katika kata 14 ambapo jamii imefanikiwa kupata elimu katika nyanja ambali mbali ikiwemo ufundi, uashi, makenika pamoja na mambo ya umeme.
Kadhalika amesema kwamba Halmashauri ya Kibaha mji imeendelea kutekeleza agizo la Rais Samia la kutenga asilimia 10 yanayotokana na mapato yake ya ndani, kwa kila mwaka kwa ajili ya kuwaapatia makundi ya wanawake, vijana pamoja na watu wenye ulemavu kwa lengo la kuweza kuwawezesha kichumi.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi (CCM) Mwajuma Nyamaka amewapongeza wanawake na kuwataka kuhakikisha kwamba wanajiandaa kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 ikiwa pamoja na kumpa sapoti Rais Samia Suluhu ili aweze kushinda kwa kishindo katika uchaguzi huo.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Dangini Mfaume Kalanguti wamewahimiza wazazi na walezi kuhakikisha kwamba wanaweka misingi mzuri ya kuchapa kazi kwa bidii na kuachana na kuwa tegemezi ikiwemo kuwalea na kuwalinda watoto katika masuala mbali mbali ya ulinzi na usalama.
Kauli mbiu ya mwaka huu ya siku ya mwanamke Duniani inasema kwamba Wanawake na wasichana tuimarishe Haki, usawa na uwezeshaji ambapo pia imeambatana na maonesho mbali mbali kutoka kwa wajasiriamali wa Halmashauri ya Kibaha mji.