
*Kupata elimu ya kudai haki zao pindi zinapokiukwa na watoa huduma.
Na Chalila Kibuda ,Michuzi TV
MAADHIMISHO ya Siku ya Haki ya Watumiaji Duniani ambayo hufanyika Machi 15ya kila Mwaka imetajwa kuwa ni muhimu katika kujenga uelewa wananchi katika kujua haki zao za utumiaji wa huduma mbalimbali.
Maadhimisho haya yatafanyika mkoani Morogoro machi 15.
Akizungumza na Waandishi wa habari Mwenyekiti wa Jukwaa la Watumiaji Tanzania (TCF) Daud Daudi amesema kuwa wadau wa watumiaji wamekuwa hawana uelewa unaofanya kukosa haki zao pindi wanapokutana changamoto za kupata huduma katika baadhi ya Taasisi za Serikali pamoja na Sekta binafsi.
Amesema kuwa watumiaji wa huduma wana haki zao za msingi kukiukwa kwa taratibu za kupata huduma ni haki yao kutoa taarifa kwa taasisi zitazofanya huduma kwa malengo ya maendeleo ya taifa.
Daudi amesema Tanzania ina mabaraza manne ya watumiaji wa huduma ambapo wananchi wakiwa na changamoto wanatakiwa kutoa taarifa katika kuboresha huduma hizo.
Mabaraza hayo ni EWURA CCC,TCRA CCC,TCAA CCC pamoja na LATRA CCC ambapo kazi ya mabaraza hayo ni kusimamia watoa huduma kuhakikisha watumiaji hawapati changamoto ya upatikanaji wa huduma.
Amesema wananchi washirika maadhimisho hayo ya kujifunza haki za watumiaji na junsi ya kutumia huduma salama kwa Kauli mbiu ya Haki na Maisha Endelevu kwa Mtumiaji
Hata hivyo amesema maadhimisho hayo yanakusudia kuhamasisha matumizi endelevu ya rasilimali kwa kuwa na majadiliano kati ya watimiaji ,watoa huduma na wadau wa maendeleo.
Amesema lengo jukwaa hilo ni kulinda haki za watumiaji na kuhimiza matumizi salama na endelevu ya huduma pamoja na kupata elimu kuhusu haki zao huku serikali na wadau wa sekta husika wakihimizwa kuhakikisha huduma bora na za haki zinapatikana kwa wote .
“Mtumiaji anapaswa kuwa na nguvu ya kufanya maamuzi sahihi kupata huduma salama, nafuu ,endelevu ,kila mtu ana haki ya kuishi katika jamii inayowajibika kulinda mazingira na rasilamali kwa vizazi vijavyo “amesema Daudi
Amasema TCF inatilia mkazo matumizi salama ya huduma katika sekta ya Nishati,Mawasiliano,Usafiri wa Anga pamoja na Usafiri wa Nchi Kavu huku serikali ikilenga kuhakikisha kuwa ifikapo 2034 asilimia 80 ya Watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia “Tusibaki nyuma katika mabadiliko haya .kutumia nishati safi si tu kwa faida ya leo bali kwa afya na ustawi wa kesho”
Nae Katibu Mtendaji wa TCRA CCC Mary Msuya amesema usalama wa mtumiaji wa mtandaoni ni ajenda muhimu mwaka huu kwa kuhimiza faragha na matumizi salama ya huduma za kidijitali.