Na Mwandishi Wetu,Michuzi TV
Maybelline New York, bidhaa inayoongoza duniani katika ulimwengu wa vipodozi, inajivunia kutangaza uzinduzi wake rasmi nchini Tanzania, hatua inayofungua msimu mpya wa upatikanaji wa urembo wa hali ya juu kwa wote.
Uzinduzi huo umefanyika katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ikiwa ni sherehe ya kujieleza, kujiamini, na ujumuishi, ikiimarisha dhamira ya Maybelline ya kuwawezesha wanawake kupitia nguvu yavipodozi.
Hafla kubwa ya uzinduzi ilifanyika katika Milimani City Mall Kioski, Jijini Dar es Salaam ambapo wateja wa Tanzania walipata fursa ya kujifunza na kujionea wenyewe bidhaa mbalimbali za Maybelline.
Bodhaa hizo ni pamoja na foundations zinazofaa kwarangi zote za ngozi, rangi nzuri za midomo, na mascara maarufu za bidhaa hiyo kwa kuleta urembo wa kiwango cha juu kwa bei nafuu na kwamba Maybelline inalenga kuifanya hudumaya kitaalamu ya vipodozi na urembo ipatikane kwa kilamtu.
Zaidi ya kuwa uzinduzi wa bidhaa, hafla hiyo inaashiriadhamira ya Maybelline ya kuthamini upekee wa kila mtuna kuleta mageuzi katika viwango vya urembo. Upanuzi wa upatikanaji wa bidhaa hiyo hadi Tanzania unamaanisha kuwa wateja sasa wataweza kufurahia bidhaa za urembo zilizoandaliwa mahsusi kukidhi mahitaji yao ya kipekee.
Uzinduzi huu pia unaangazia dhamira ya Maybelline yakuhakikisha upatikanaji wa bidhaa kwa urahisi. Sasa, bidhaa za Maybelline zinapatikana kwa bei nafuu katikamaduka ya SH Amon pamoja na Maybelline kiosk ililopoMilimani City Mall, kuhakikisha wapenzi wa urembo kotenchini wanaweza kufikia bidhaa kwa urahisi.
Hata hivyo katika uzinduzi huo vyombo vya habari na wapenzi wa urembo wamepata uzoefu wa moja kwa moja wa bidhaa za Maybelline, ikisisitiza ujumbe wa bidhaa wa “urembo usio na mipaka.”
“Maybelline New York ni zaidi ya vipodozi—nikuhusu kujiamini, ubunifu, na kujieleza. Kuingia kwetukatika soko la Tanzania ni hatua muhimu katika kuhakikisha bidhaa za urembo za ubora wa hali ya juu zinapatikana kwa watu wengi zaidi, tukiwahamasisha wakubali uzuri wao wa kipekee,” amesema Debra Killingo, Meneja – Maybelline New York.
Wakati huo huo Meneja Mkuu wa L’Oreal Afrika Mashariki Victoria Karanja amesema baada ya uzinduzi huo bidhaa za Maybelline zitapatikanakatika maduka ya SH Amon na Milimani City Mall Kiosk, kwa ajili ya kuwezesha wateja wa Tanzania kufikia vipodozi vyenyeubora wa juu kwa urahisi zaidi kuliko hapo awali.
Ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa mwanamke pamoja na mambo mengine anatakiwa kujiamini kwa kuwa mrembo na uwepo wa bidhaa hizo za urembo sasa mwanamke wa Tanzania anakwenda kuwa mrembo zaidi huku Akieleza pia uwepo wa duka hilo kunakwenda kuongeza fursa ya ajira kwa watanzania.
Kuhusu Maybelline New York ni bidhaa namba moja ya vipodozi duniani, inayotoa bidhaa za urembo za hali ya juu zinazoendana na mitindo ya kisasa na inapatikana katika nchi zaidi ya 120. Maybelline inaendelea kujikita katika ubunifu, ujumuishi, na kuwawezesha watu kujieleza kupitia vipodozi.