Na Oscar Assenga,TANGA
SHIRIKA la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limepongeza kutokana na juhudi zake kubwa za kutoa elimu kwa wananchi wakiwemo wadau mbalimbali juu ya madhara yatokanayo na uchafuzi wa mazingira ya bahari ambayo yanaweza kuelekea athari za kiuchumi kwa mtu moja moja na Taifa kwa ujumla.
Pongezi hizo zimetolewa leo na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Balozi Dkt.Batilda Buriani wakati akifungua warsha ya mpango wa Taifa wa kujiandaa na mapambano ya umwagikaji wa mafuta katika bahati na mafuta.
Ambapo alisema licha ya sekta ya uchumi kuathirika kuna uwezekano mkubwa wa kupotea kwa viumbe vya bahari endapo juhudi mbalimbali hazitafanyika.
Aidha alisema kwamba jamii inapaswa kutambua umwagikaji wa mafuta katika bahari na maziwa unaweza ukaathiri vyanzo vya mapato ya wananchi wakiwemo wavuvi na hivy kuathiri uchumi wa mtu mmoja mmoja lakini Taifa kwa ujumla
“Niseme tu kwamba Semina hii ina umuhimu mkubwa kwani mafuta yatakapo mwagika watu tunategemea mazao ya baharini tutapata hasara Tanga tumeshaanza na kujikita katika zao la Mwani hivyo kukitokea dharura yeyote ni lazima kuwa tayari kukabiliana nayo hivyo ni lazima tujiandae kimafunzo na kivifaa.
“Kwa kweli tunalipongeza shirika la TASAC kwa juhudi mbalimbali inazozifanya ikiwemo kutoa elimu jumuishi pamoja na ugawaji wa vifaa vinavyoweza kutumika wakati wa dharuraniwatake kuendelea kuongeza elimu hiyo kwa wadau wakiwemo wananchi sambamaba na kuwa na vifaa vya kutosha”Alisema
Hata hivyo alitumia wasaa huo kusifu juhudi za shirika hili la kutoa vifaa vya kukabiliana na changamoto hizo huku akitaka lazima wawe na utaribu mzuri wa kuvitumia ili kuweza kufikiwa kwa urahisi ili oparesheni ikitokea iwe rahisi kuvipata.
Alisema mkoa umejipanga kutoa elimu kwa wadau wote wa bahari pamoja na wananchi jinsi ya kutumia vifaa vitakavyotumika wakati wa kupambana na dharura ya umwagikaji wa mafuta hii ikilenga kuongeza zaidi ushirikiano katika kupambana na majanga pale yatakapotokea.
“Bandari ya Tanga hususani eneo la Chongoleani linatarajiwa kuwa lango kuu la kupokea na kusafirisha mafuta ghafi kutoka Hoima Uganda hadi Tanga Chongoleani , ujenzi wa bomba hilo upo katika hatua za mwisho wenzetu tayari wameshaweka matank ya kuhifadhia mafuta, Mkoa una mashamba ya mafuta umeyatenga tumeshatenga vitalu ambapo wenzetu wa makampuni makubwa wana maeneo yao”
“Umuhimu wa hii semini ni mkubwa sana mafuta yatakapo mwagika watu tunategemea mazao ya baharini tutapata hasara Tanga tumeshaanza na kujikita katika zao la Mwani hivyo kukitokea dharura yeyote ni lazima kuwa tayari kukabiliana nayo hivyo ni lazima tujiandae kimafunzo, kivifaa.
Awali akizungumza Mkurugenzi wa Idara ya Usalama, Ulinzi na Utunzaji wa mazingira kutoka TASAC Leticia Mutaki alisema kuwa katika kuendelea kudhibiti na kupambana na athari za kimazingira katika bahari shirika hilo linaendelea kutekeleza mpango wa kitaifa wa umwagikaji wa mafuta.
Ambapo alisema mpango huo unahusisha wadau mbalimbali pamoja na wananchi katika ngazi za wilaya hii ikiwa na lengo la kuongeza uelewa na itayati wa kupambana na majanga yanapotokea.
Aidha Mutaki alisema kuwa TASAC inaendelea kusiamamia usalama wa vyombo vyote vinavyofanya safari katika bahati kuhakikisha vinakuwa na ubora wakati wote hii ikiwa na lengo la kupambana na athari za kimazingira ambazo zinaweza kujitokeza na kuelekea athari kwa viumbe na rasilimali nyingine zinazopatikana baharini.
“Pia tunashughulika na usalama wa vyombo vinavyopita kwenye maji tunaviangalia ili visichafue mazingira yetu sasa hivi tuna suala la uchumi wa buluu ambao sasa hivi Duniani imeelekeza kwamba Kuna maliasili nyingi kwenye maji lazima tuvune kwa namna ambayo itaweza kuwa endelevu TASAC tunawajibu wa kuhakikisha kwamba maliasili zote zilizopo kwenye maji zinabaki salama”
Alisema wamekuja mkoani hapa kujenga timu ili kunatokea bahati mbaya ya umwagikaji wa mafuta ili wawe na watu ambao wanaweza kufanya nao kazi katika kudhibiti athari zianazoweza kujitokeza kutokana na mafuta mabayo yanavuja.
“Tunao mradi wa EACOP ambao unaosafirisha mafuta kutoka kule Hoima Uganda hadi Tanga Tanzania kama itatokea dharira yeyote ya umwagikaji wa mafuta ili kuweza kupunguza athari za kimazingira” Alisema.
Hata hivyo Mwakilishi kutoka shirika la bandari Zanzibar Abubakar Ally amelipongeze shirika la uwakala wa Meli Tanzania ‘TASAC’ kutokana na mafunzo hayo ambayo wameendelea kuyatoa kwa wadau wa usafirishaji wa majini pamoja na wananchi ambapo matokeo yake yameonekana na kufanikiwa kwa asilimia kubwa.