Matukio ya picha mbalimbali katika uzinduzi wa namba 180 ya kupiga bure katika huduma za dharula
Naibu Waziri wa Nishati Judidh Kapinga akizungumza wakati wa uzinduzi wa namba 180 ya kupiga bure katika dharula ya huduma ya umeme ,jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga akitoa maelezo kuhusiana na maboresho ya Shirika hilo kuleta namba 180 ya kupiga bure katika dharula za Umeme
*Watapiga namba 180 bure wakati wa dharula
Na Chalila Kibuda,Michuzi TV
SERIKALI imesema kuwa kitendo cha Shirika la Umeme Tanzania kutengeneza namba ya 180 ya kupiga bure katika dharula ya huduma ya umeme imepunguza mzigo kwa kwa wananchi.
Hayo amesyasema Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga katika hafla ya uzinduzi wa namba 180 ya kupiga bure katika dharula ya huduma ya umeme nchini.
Amesema kuwa namba ya kupiga bure ni hatua muhimu katika maboresho ya huduma kwa wateja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na kurahisisha mawasiliano kati ya TANESCO na wateja wake, huku ukihakikisha changamoto zinatatuliwa kwa haraka na kwa ufanisi zaidi.
Amesema kuwa huo ni utekelezaji wa agizo la Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko, aliyesisitiza umuhimu wa kuwa na namba ya bure kwa wateja ili kuboresha utoaji wa huduma. Kupitia namba hii, wateja wa TANESCO wataweza kupata msaada wa haraka kuhusu matatizo ya umeme, bili, na huduma nyinginezo bila gharama yoyote.
Akizungumza mara baada ya kuzindua huduma hiyo, Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Judith Kapinga aliwataka Mameneja wa Mikoa na Wilaya wa TANESCO kuhakikisha huduma kwa wateja inaboreshwa kupitia usimamizi madhubuti wa mfumo huo mpya. Pia aliwahimiza wananchi kuitumia namba hiyo kwa malengo sahihi, akisisitiza kuwa serikali ya Awamu ya Sita inajidhatiti kuhakikisha huduma za umeme zinapatikana kwa uhakika na ubora.
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya TANESCO, Balozi Zuhura Bundala, alieleza kuwa maboresho ya huduma kwa wateja ni moja ya vipaumbele vya shirika hilo, kwani maendeleo ya kiuchumi yanategemea upatikanaji wa umeme wa uhakika.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mha. Gissima-Nyamo Hanga, alisema kuwa katika dunia ya sasa ya ushindani wa kibiashara, ni muhimu kuhakikisha wateja wanapata huduma bora na changamoto zao zinatatuliwa kwa haraka.
Uzinduzi wa namba hii ya bure ni moja ya juhudi za TANESCO kuboresha huduma kwa wateja wake na kuimarisha mfumo wa mawasiliano na wananchi.