KAMATI ya Kudumu ya Bunge Miundombinu imeshauri Serikali ujenzi wa barabara ya kutoka Tanga-Pangani –Bagamoyo upitie katika eneo la Hifadhi ya Taifa ya Saadani ili kufungua mkoa huo kiuchumi na kuongeza idadi kubwa ya watalii.
Ushauri huo wa Kamati ulitolewa leo na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Moshi Kakoso mara baada ya kamati hiyo kutembelea ujenzi wa barabara ya Tanga-Pangani pamoja na kukagua ujenzi wa Daraja la Mto Pangani
Alisema kwa sababu Serikali haijengi barabara kuwafurahisha wananchi bali kuufungua uchumi wa nchi sasa kama wanapeleka barabara na kuichepusha kwenye eneo ambalo lingekuwa na tija zaidi wanaomba hilo walifanyie upembuzi yakinifu huko serikali na wapate majibu ya msingi yenye ufanisi kwenye miradi ambayo ni ya kimkakati.
“Kujenga barabara hiyo wangeiacha na Serikali iliamua kujenga barabara upande wa ufukweni pembezoni mwa bahari ili ilete maendeleo kwa wananchi wa maeneo hayo sasa hawakatai kile kipande ambacho kimepita huko hivyo nendeni mkakae kile kipande ambacho kitakuwa kimebaki cha kukatisha pale nendeni mkakae mkiingize kwenye mfumo ambao mtaujua nyie”Alisema
Mwenyekiti hiyo alisema kwamba wakakae Wizara na Ofisi ya Makamu ya Rais ili kuangalia uwezekano wa barabara hiyo iweze kuifungua iende eneo la Hifadhi ya Taifa ya Saadan na kuweza kuufungua ushoroba wa utalii pamoja na kuifungua kiuchumi mkoa wa Tanga na Taifa kwa ujumla.
“Mhe Naibu Waziri tunawapongeza kwa ujenzi unaoendelea wa daraja ni mzuri na maendeleo ya mradi wa daraja bunge limeridhishwa na litakapokamilika litaleta sura nzuri kwenye maeneo ya wilaya ya Pangani na mkoa na litakuwa kivutio na daraja pekee ambalo litakuwa juu sana na wanaona serikali uwekezaji wake utakuwa na tija zaidi”Alisema Mwenyekiti huyo wa kamati.
Hata hivyo akizungumza wakati akihitimisha ziara ya kamati hiyo aliishauri Serikali kuhakikisha inakamilisha haraka barabara ya Tanga-Pangani ili kuepusha serikali kutokuingia gharama nyengine za kulipa fidia.
Alisema kwamba uwekezaji unaowekezwa katika Daraja la Mto Pangani hautakuwa na maana iwapo barabara unganishi haitakuwepo huku akitaka lifanyiwe kazi kuhakikisha wanakamilisha ujenzi huo ili uende sambamba na daraja.
Hata hivyo aliiomba Serikali iwasimamie wakandarasi waweze kukamilisha ujenzi wa barabara kwa mujibu wa mkataba ambao mlishakubaliana nao wabunge wamehoji kuna wasiwasi kwamba ile miezi minne kwamba wanaweza kukamilisha kipande cha barabara na wasipowasimamia wataongeza muda mwengine wa ziada.
“Simamieni kile kipande kikamilike kije kuunga kwenye eneo la Barabara narudi kusema Bunge lingependa barabara ya Kutoka Tanga ingeenda kupitia eneo la Hifadhi ya Saadani wangekuwa wameufungua mkoa kiuchumi na kuongeza idadi ya watalii”Alisema
Awali akizungumza Naibu Katibu Mkuu wizara ya Ujenzi Msonde wataendelea kufuatilia kuona wapi inakwama na nni kifanyike
Msimamizi wa Barabara ya Tanga-Pangani kutoka Wakala wa Barabarani nchini (Tanroad) Mkoa wa Tanga Mhandisi Godson Yohana alisema daraja la Mto Pangani lina urefu wa mita 525 ambapo kwa miradi ya madaraja nchini hilo ni daraja la pili kwa ukubwa na la kwanza ni Kigongo Busisi Mwanza.
Alisema ujenzi wa mradi huo ulianza Desemba 7 mwaka 2022 na gharama za mradi Bilioni 82.2 na unatekelezwa na Kampuni ya Shandon Likway Group ya kutokea nchini china na ujenzi huo umefikia asilimia 55 na unahusisha barabara na ujenzi wa daraja.
Mhandisi huyo alisema kwamba nguzo zote za kushika daraja zimekwisha kamilika na wanaendelea na ujenzi na mkandarasi yupo eneo la mradi huku akieleza ujenzi wa barabara loti ya kwanza umefikia asilimia 75 na mkandarasi mpaka sasa amekamiisha kipande cha kiliomita 15.8.
Alisema changaoto kubwa iliyowachelewesha kwenye mradi huo ni upatikanaji wa jiwe lenye sifa ya kutumika kwa lami ambayo wanaiweka hapo kutokana na uwepo wa teknolojia mpya kwamba mawe yanayotumika kusagia kokoto yanatakiwa kuwa na nguvu na viwango vya juu.
“Jiwe hilo tumelipata Muheza kilimota 60 kutoka eneo la mradi na walikuwa na leseni za watu wanaoyamiliki ilikuwa na changamoto kidogo lakini yamekamilila mradi huo unatarajiwa kukamilika 16June 2025”Alisema
Hata hivyo alisema kilomita zilizobaki ni 34 ambapo wanaishukuru Serikali tayari imemlipa mkandarasi huyo tokea Desemba mwaka jana kiasi cha Bilioni 4.7 na mwezi wa pili mwaka huu walilipaswa Bilioni 10.8.
Alisema mwanzoni walikuwa na changamoto mbalimbali kusimama kwa mradi na wamempa wiki mbili arudi kazi na kwa sasa wanaendele kuweka vifaa ili kuendelea na ujenzi huo