Mkuu wa Wilaya ya Butiama, mkoani Mara, Mhe. Moses Kaegele, akikabidhiwa kipeperushi na Afisa Usimamizi wa Fedha, Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bw. Stanley Kibakaya, chenye mada mbalimbali ikiwemo mikopo na akiba ambazo zitafundishwa kwa wananchi wilayani humo.

Mkuu wa Wilaya ya Butiama, mkoani Mara, Mhe. Moses Kaegele, akizungumza alipokutana na Timu ya Wataalamu kutoka Wizara ya Fedha na Benki Kuu ya Tanzania (BoT), ambao walifika ofisini kwake kujitambulisha ili kuanza kutoa elimu ya fedha kwa wananchi katika maeneo mbalimbali wilayani humo.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Butiama, mkoani Mara, Bi. Mbuke, akikabidhiwa kipeperushi na Afisa Usimamizi wa Fedha, Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bi. Elizabeth Mnzava, chenye mada mbalimbali ikiwemo mikopo na akiba ambazo zitafundishwa kwa wananchi wilayani humo.
Mkuu wa Wilaya ya Butiama, Mhe. Moses Kaegele, akiteta jambo na Timu ya Wataalamu kutoka Wizara ya Fedha na Benki Kuu ya Tanzania (BoT), ambao walifika ofisini kwake kujitambulisha ili kuanza kutoa elimu ya fedha kwa wananchi katika maeneo mbalimbali wilayani humo. Kutoka kushoto ni Afisa Sheria Mwandamizi, Idara ya Ustawi na Huduma Jumuishi za Fedha, Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Ramadhani Myonga, Afisa Usimamizi wa Fedha, Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bw. Stanley Kibakaya na Afisa Usimamizi wa Fedha, Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bi. Elizabeth Mnzava.


Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Butiama, mkoani Mara, Bi. Mbuke, akizungumza alipokutana na Timu ya Wataalamu kutoka Wizara ya Fedha na Benki Kuu ya Tanzania (BoT), ambao walifika ofisini kwake kujitambulisha ili kuanza kutoa elimu ya fedha kwa wananchi katika maeneo mbalimbali ya Halmashauri hiyo.

Mkuu wa Wilaya ya Butiama, mkoani Mara, Mhe. Moses Kaegele, akizungumza alipokutana na Timu ya Wataalamu kutoka Wizara ya Fedha na Benki Kuu ya Tanzania (BoT), ambao walifika ofisini kwake kujitambulisha ili kuanza kutoa elimu ya fedha kwa wananchi katika maeneo mbalimbali wilayani humo. Kutoka kulia ni Afisa Usimamizi wa Fedha, Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bi. Elizabeth Mnzava, Afisa Sheria Mwandamizi, Idara ya Ustawi na Huduma Jumuishi za Fedha, Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Ramadhani Myonga na Afisa Usimamizi wa Fedha, Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bw. Stanley Kibakaya.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya elimu ya fedha wakazi wa Kijiji Kyankoma, Kata ya Nyamimange, Wilaya ya Butiama, mkoani Mara, wakiangalia filamu yenye mada mbalimbali ikiwemo masuala ya mikopo, akiba na uwekezaji wakati wa mafunzo ya elimu ya fedha yaliyotolewa na Wataalamu kutoka Wizara ya Fedha na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) mkoani Mara.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WF, Butiama Mara)