Mkurugenzi Mtendaji wa Bank of Africa Tanzania, Esther Maruma (kushoto) akizungumza katika mkutano wa kuchochea kasi ya maendeleo ya Wanawake (Accelerate Women Summit 2025) uliofanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni, katikati ni ni Mkurugenzi wa Trademark Kanda ya Africa Mashariki na Kati, Monica Hangi na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Yono, Scolastika Kevela.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bank of Africa Tanzania, Esther Cecil Maruma(wa nne kutoka kulia) akiwa katika picha picha ya pamoja na wazungumzaji katika mkutano wawa kuchochea kasi ya maendeleo ya Wanawake (Accelerate Women Summit 2025), jijini Dar es Salaam hivi karibuni
BANK of Africa Tanzania, imekuwa mshirika wa mkutano wa kuchochea kasi ya maendeleo ya Wanawake (Accelerate Women Summit 2025) uliofanyika jijini Dar es Salaam na imeeleza dhamira yake ya kuwezesha wanawake wajasiriamali nchini na kuwajumuisha rasmi katika mfumo wa kifedha ikiamini kuwa Wanawake wakiwezeshwa kibiashara wataweza kuwa wabunifu,wataibua ajira na uwepo ustahimivu katika uchumi wa nchi.
Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Esther Maruma amesma wanaamini wanawake wanapofanikiwa, jamii na uchumi una stawi.
“Ushiriki wetu katika Mkutano huu wa kuchochea kasi ya maendeleo ya wanawake unadhihirisha dhamira yetu ya kutengeneza fursa muhimu kwa Wanawake wajasiriamali kupata raslimali za kifedha,ushauri na msaada wa ukuzaji wa biashara zao.” Amesema Esther
Amesema dhana hiyo inaendana na maadili yao ya msingi ya ujumuishaji, ubunifu, na kuleta mabadiliko chanya kwa kuwakikishia kuwa mbali ya kuwa taasisi ya fedha bali wataenda nao sambamba kuhakikisha wanafanikiwa na kupata maendeleo”
Amesema Benki imelenga kuondoa vikwazo vinavyokwamisha wanawake kupata huduma za kifedha na upanuzi wa biashara zao kwa kuwapatia uduma zinazoendana na matakwa yao.kuwa nao karibu na kuandaa mikutano na semina ili kuhakikisha wanapata mafanikio na biashara zao zinastawi.
mkutano wa kuchochea kasi ya maendeleo ya Wanawake (Accelerate Women Summit 2025) uliokuwa na kauli mbiu ya “Hakuna wa kumzuia Mwanamke- Unstoppable Woman”,ulilenga kuwaamsha Wanawake kuchangamkia fursa zenye kuwapeleka kwenye maendeleo ya kibiashara na Bank of Africa Tanzania inayo dhamira ya kuhamasisha mabadiliko haya, ikiwashirikisha wajasiriamali wanawake, na kukuza mfumo wa kifedha wa ujumuishaji ambapo kila mjasiriamali, bila kujali jinsia, akiwezeshwa anafanikiwa.