MKUU wa wilaya ya Ilala, mkoani Dar es salaam, Edward Mpogolo ameshiriki zoezi la kujiandikisha katika maboresho ya Daftari la kudumu la mpiga kura Kata ya Ilala, mtaa wa Karume.
Mpogolo amefika Mtaa wa Karume, majira ya asubuhi na kuungana na foleni ya wananchi wa mtaa huo ili kuhakikisha anaboresha taarifa zake katika daftari la kudumu la Mpiga kura.
Akizungumza na Wananchi wa Wilaya ya Ilala, Mpogolo amewaomba wananchi kujitokeza katika mitaa yao na kata wanazoishi vilipo vituo kwa ajili ya kwenda kujiandikisha katika Daftari la mpiga kura Mkoanib Dar es Salaam.
Amebainisha kuwa zoezi ilo la wiki moja ili liwe na mafanikio ni vema wale wenye sifa wote kujiandikisha na baadae kushiriki kumpigia kura Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta Samia Suluhu Hassan, wabunge na madiwani katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.
Mkuu wa wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, amebainisha ili uweze kupata haki ya kupiga kura kila mmoja awe amejiandisha, kwa kufuata taratibu eneo analoishi au kuboresha taarifa zake ikiwa amehama toka sehemu moja kwenye nyingine.
Aidha ametoa wito kwa Wenyeviti wa Serikali za mitaa pamoja na Wajumbe wa Serikali za Mitaa kushirikiana kwa pamoja kwenda kuhamasishana wananchi kujitokeza kujiandikisha katika vituo vyao.
Daftari la maboresho ya mpiga kura mkoa Dar es Salaam limezinduliwa Machi 17 mwaka huu na zoezi hilo linatarajia kumalizika Machi 23 /2025 .
Hayo ni maandalizi muhimu kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ajili ya uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani ambapo uchaguzi huo unafanyika kila baada miaka mitano ambapo kabla uchaguzi kufika wanachi wake lazima wawe wamejindikisha katika Daftari la mpiga kura.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Karume, Hajji Bechina, amesema katika eneo la mtaa wake zoezi linaenda vizuri toka siku ya ufunguzi mpaka sasa watu wanajitokeza kujiandikisha na hamasa ya kujiamdikisha inaendelea kwa kushirikiana na wajumbe.