Mkuu wa wilaya ya Ilala, Mkoani Dar es salaam, Edward Mpogolo amepiga marufuku shughuli zote za kilimo katika bonde la magore kibeberu kata ya Mzinga.
Hatua hiyo ya kupiga marufuku shughuli zote za kibinadamu katika bonde ilo imekuja baada ya adha ya kukatika kwa daraja na kukata mawasiliano ya pande mbili.
Mpogolo, ameeleza kuwa wakati mkandarasi anaendelea kuhakikisha mawasiliano yamerejea katika hali ya kawaida, utekelezaji wa agizo unaanza mara moja.
Akizungumza na viongozi wa serikali ya mtaa, wananchi na baadhi ya wakulima, Mpogolo amesisitiza sheria za matumizi ya ardhi kwa kuzingatia mita sitini toka barabara inapoanzia.
Mpogolo, amewaeleza athali za kilimo katika bonde ilo ni pamoja na kutanuka kwa mto, hali inayofanya mto kuhama katika njia yake ya asili na kusababisha maji kupita nje ya makaravati.
Mkuu huyo wa wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, ametumia nafasi hiyo kumsisitiza Mkandarasi kuhakikisha anazibua njia zote za maji ili kurudisha mifumo sahihi ya maji.
Kwa upande wake diwani wa kata ya Mzinga, Isac Job amemshukuru Mkuu wa wilaya kwa hatua za haraka alizochukua kuhakikisha mawasiliano katika eneo ilo yanarejea.
Huku Meneja wa TARURA Wilaya ya Ilala Eng. Magore amemwakikishia Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, kusimamia usiku na mchana ujenzi wa daraja ilo ili wananchi, na watumiaji wengine waendelee kupata huduma muhimu ya mawasiliano.
Pamoja na kutoa wito kwa madereva wa magari makubwa kutopitisha magari na mizigo yasiyoendana na uzito wa daraja la magore.