KAMPUNI ya bia Tanzani (TBL) , imetenga wiki zima ya kuadhimisha wiki ya maji. Ambapo jana mefadha hafla ya maadhimisho katika kiwanda chao cha bia kilichopo Arusha.
Maadhimisho haya yamelenga kutambua umuhimu wa maji katika uzalishaji wa bidhaa za TBL na na kwa matumizi ya kawaida ya jamii.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo” Mkurugenzi wa maswala ya sheria na mahusiano ya kampuni ya TBL, Bi. Neema Temba amesema kuwa kwa mika mitano iliyopita wamefanikiwa kupunguza matimizi ya maji katika uzalishaji kwa asilimia 30%, mafanikio haya yametokana na uwekezaji katika teknolojia za urejereaji wa maji pamoja na uboreshaji qa mifumo ya uzalishaji.
Naye mkuu wa wilaya ya Arusha, Mheshimiwa Joseph Mkude, amipongeza kampuni ya TBL kwa juhudi zake za kuhakikisha wanakuwa na matumizi bora ya maji. Amesema
“Maji ni rasilimali muhimu sana kwa jamii hasa katika kuchochea ukuaji wa uchumi na kuboresha maisha ya watu. Nawapongeza TBL kwa kuwa msitari wa mbele kuhakikisha rasimali hii muhimu inatuzwa ili kuweza kukabiliana na changamoto za utoshelevu wa maji hapa nchini.
Hata hivyo katika maadhimisho haya TBL waliandaa majadiliano maalumu na wadau mbambali wakiwemo OIKOS na WWF ambayo yalilenga kupeana mbinu bora za kupunguza matumizi ya maji katika uzalishaji na kuIngatia ubora wa bidhaa.