Na Mwandishi wetu Dodoma
Mkurugenzi Mtendaji Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) Bwana Joel Laurent amesema moja ya mfanikio ya tasnia ya mbolea ni ongezeko la aina za mbolea zinazopatikana sokoni na kuwapa wakulima fursa ya kuchagua mbolea kulingana na mahitaji ya udongo na mazao wanayolima ambapo katika kipindi cha miaka 4 ya Dkt Samia mbolea zilizosajiliwa na kuruhusiwa kutumika nchini zimeongezeka kufikia 612 ikilinganishwa na mbolea 350 zilizokuwa zimesajiliwa mwaka 2020/2021.
Mkurugenzi huyo amesemea hayo leo Jijini Dodoma Machi 19,2025 katika Mkutano na Wanahabari akielezea mafanikio ya Mamlaka hiyo katika kipindi cha Miaka 4 ya Uongozi wa awamu ya sita.
Amesema kuwa biashara ya mbolea nchini imekua kwa kiasi kikubwa ambapo wafanyabiashara wa mbolea waliopewa leseni wameongezeka kutoka 3,069 mwaka 2020/21 hadi 7,302 Februari, 2025.
Aidha, upatikanaji wa mbolea umeongezeka kutoka tani 766,024 mwaka 2020/2021 hadi tani 1,213,729 mwaka 2023/2024, uingizaji wa mbolea umeongezeka kutoka tani 504,122 mwaka 2020/2021 hadi tani 728,758 mwaka 2023/2024 na uzalishaji wa ndani umeongezeka kutoka tani 42,695 mwaka 2020/2021 hadi tani 158,628 mwaka 2023/2024.