• Mpango wa siku 60 wenye mkondo wa ubunifu na matukio ya kiteknolojia za kidigitali
• Mada zinajumuisha uzoefu wa wateja, utambulisho wa kidijitali, na bidhaa za kidijitali
• Biashara changa (startups) zilizochaguliwa zitapata fursa ya kujaribu suluhisho zao na Benki ya Absa Tanzania
• Kila startup iliyochaguliwa itapata ufikiaji wa bidhaa za kiteknolojia zenye thamani ya USD 600,000
• Mpango utakamilika kwa siku ya majaribio, inayotoa fursa ya kuunganishwa na wawekezaji wa ndani na wa kimataifa
Benki
ya Absa Tanzania, kwa kushirikiana na Hindsight Ventures, imezindua
Wazo Challenge Tanzania, mpango wa kipekee unaolenga kuimarisha ubunifu
na ujasiriamali katika sekta ya Teknolojia ya Fedha (FinTech), na
biashara changa (startup) nchini Tanzania.
Hafla ya uzinduzi,
iliyofanyika jijini Dar es Salaam Jana na kuhudhuriwa na Mgeni Rasmi,
Bw. Kennedy Komba, Mkurugenzi wa Uendelezaji wa Kifedha na Ujumuishaji
wa Kibenki kutoka Benki Kuu ya Tanzania, akimwakilisha Gavana.
Ikiwa
na kaulimbiu “Benki ya Siku Zijazo” au “Bank of the Future”, Wazo
Challenge Tanzania inakaribisha biashara changa katika Teknolojia ya
Fedha za (FinTech) na wabunifu kuwasilisha suluhisho bunifu zinazoweza
kufanikisha mabadiliko makubwa katika sekta ya kibenki.
Mpango
huu ni sehemu ya ushirikiano wa miaka mitatu kati ya Benki ya Absa
Tanzania na Hindsight Ventures, ukiwa na lengo la kusaidia ukuaji wa
ujasiriamali na kuongeza upanuzi wa startups nchini.
Akizungumza
katika uzinduzi huo, Bw. Obedi Laiser, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya
Absa Tanzania, alisisitiza dhamira ya benki hiyo katika kukuza ubunifu
na ujumuishaji wa kifedha. “Wazo Challenge Tanzania ni uthibitisho wa
imani yetu katika nguvu ya ubunifu kwenye kuleta maendeleo na thamani
kwa wateja wetu – na hii inaenda sambamba na lengo kuu la benki yetu
ikiwa ni “Kuiwezesha Afrika ya kesho, pamoja, hatua moja baada ya
nyingine.” na Ahadi ya chapa yetu “Stori yako ina thamani”. Tunafurahia
kushirikiana na Hindsight Ventures kuwawezesha wabunifu na wajasiriamali
wa Tanzania.”
Bw. Ajay Ramasubramaniam, Mwanzilishi Mwenza na
Mkurugenzi Mtendaji wa Hindsight Ventures, aliunga mkono kauli hiyo,
akisema, “Tunatarajia kufanya kazi na Benki ya Absa Tanzania ili
kuimarisha mfumo wa FinTech wa ndani kupitia mbinu iliyopangiliwa ya
kugundua na kushirikiana na bidhaa na suluhisho bunifu. Startups na
wabunifu watanufaika kwa kupata ufikiaji wa mtandao wa Absa, pamoja na
mtandao wetu wa kimataifa wa FinTech, na tunahisi kuwa hii itakuwa hatua
muhimu kwa sekta hii.”
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Huduma
Jumuishi za Fedha kutoka Benki Kuu ya Tanzania, Bwana Kennedy Komba,
akimwakilisha Gavana, alipongeza benki ya Absa Tanzania kwa kuja na Wazo
Challlenge huku akisema ni moja ya njia ya kuhamashisha matumizi ya
teknolojia nchini.
Mpango huu unalenga kufanya huduma za benki
kuwa rahisi zaidi na zinazozingatia mahitaji ya wateja, kwa kutumia
maendeleo ya mabadiliko ya kidijitali ili kukidhi matarajio ya wateja wa
kisasa.
Mpango huu pia utatoa fursa kwa biashara changa za
teknolojia ya fesha kushirikiana na Benki ya Absa Tanzania kupitia
ushauri, ushirikiano, na uwekezaji. Kuingia kwenye mpango huu usio na
ada kutategemea kukamilisha mchakato wa kufuzu na ukaguzi wa historia.
Zaidi
ya hayo, Wazo Challenge Tanzania itatoa ufikiaji kwa wataalam wa sekta,
wakufunzi, na washauri kusaidia wenye biashara changa katika safari yao
ya kuanzisha na kukuza biashara zao. Mpango huu pia unalenga
kuunganisha biashara changa zilizochaguliwa na mtandao wa kimataifa wa
wataalam wa FinTech na wawekezaji, wanaotaka kusaidia ukuaji wa sekta ya
Teknolojia ya Fedha nchini Tanzania.
Mfumo wa FinTech wa
Tanzania umeendelea kukua kwa kasi, huku biashara kadhaa za ndani
zikivutia uwekezaji wa mitaji na kushughulikia mahitaji ya wateja.
Programu
kama Wazo Challenge Tanzania zina nafasi muhimu katika kusaidia mfumo
huu, kwa kuhamasisha ubunifu katika suluhisho za fedha za kidijitali,
ufadhili wa mnyororo wa ugavi, huduma za malipo, upimaji wa mikopo, na
uwezeshaji wa mnyororo wa thamani.
Toleo la “Benki ya Siku
Zijazo” la Wazo Challenge litahitimishwa kwa Siku Maalum ya Uoneshaji wa
Ubunifu wa Kazi, itakayofanyika kwa mwaliko maalum, ambapo washindi wa
fainali watapata nafasi ya kuwasilisha suluhisho zao za FinTech mbele ya
jopo la wawekezaji na viongozi wa sekta.
Wazo Challenge Tanzania
itaendelea kutoka 2025 hadi 2027, huku Benki ya Absa Tanzania na
Hindsight Ventures wakitoa programu za mafunzo, ushauri na ufadhili ili
kuhakikisha mafanikio ya wenye biashara changa na wabunifu wanaoshiriki.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa
Tanzania, Bw. Obedi Laiser (kulia) akishikana mikono na Mkurugenzi wa
Huduma Jumuishi za Fedha wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Kennedy
Komba jijini Dar es Salaam jana, wakati wa hafla ya uzinduzi wa mpango
wa Wazo Challenge Tanzania, unaolenga kuimarisha ubunifu na
ujasiriamali katika sekta ya Teknolojia ya Fedha (FinTech) na biashara
changa (startup) nchini Tanzania. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja na Huduma za Kidigitali, Bw. Samuel Mkuyu.
Mjumbe
wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Peter Ulanga (
kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Obedi
Laiser na Mkurugenzi wa Huduma Jumuishi za Fedha wa Benki Kuu ya
Tanzania (BoT), Bw. Kennedy Komba, wakielekea katika hafla ya uzinduzi
wa mpango wa Wazo Challenge Tanzania, unaolenga kuimarisha ubunifu na ujasiriamali katika sekta ya Teknolojia ya Fedha (FinTech) na biashara changa (startup) nchini Tanzania. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Obedi Laiser ( wa pili kulia)
akizungumza na Muanzilishi Mwenza na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya
Hindsight Ventures, Bw. Ajay Ramasubramaniam ( wa pili kushoto),
Mkurugenzi wa Huduma za kibenki Kidigitali kutoka Absa Group, Bw.
Tawanda Chatikobo (kushoto), na Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja
na Huduma za Kidigitali, Bw. Samuel Mkuyu, wakati wa hafla ya uzinduzi
wa mpango wa Wazo Challenge unaolenga kuimarisha ubunifu na ujasiriamali katika sekta ya Teknolojia ya Fedha (FinTech) na biashara changa (startup) nchini Tanzania. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar Es Salaam jana
Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Obedi Laiser akizungumza
wakati wa hafla ya uzinduzi wa mpango wa Wazo Challenge Tanzania.
Mkurugenzi
wa Huduma Jumuishi za Fedha wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Kennedy
Komba akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Wazo Challenge
Tanzania, mpango unaolenga
kuimarisha ubunifu na ujasiriamali katika sekta ya Teknolojia ya Fedha
(FinTech) na biashara changa (startup) nchini Tanzania.