Mwenyekiti wa Taasisi ya Ramadhan Charity Program 2025 Ahmed Misanga Amesema huu ni mwaka wa 8 wakitoa Sadaka ya Iftar kwa makundi mbalimbali hasa watu wenye uitaji.
Kauli hiyo ameitoa wakati wa kukabidhi swadaka ya Iftar kwenye Tasisi za kidini hapa Manispaa ya Singida, kuwa kutoa ni moyo hakuhitaji uwe na mali nyingi, na namna ya kuoneana huruma endapo mwenzako unamuona hana kitu basi unaweza kumsaidia.
“Mimi na wezangu hatuna pesa nyingi sana ila tunajichanga tunacho kipata na sisi tunaenda kusaidia watu wenye uhitaji ili wawe na furaha kama sisi ivyo tuwe watu wa kutoa sadaka nijambo jemaa sana kwa mwenyezi mungu.
Huku kwa upande wake Kaadhi wa Mkoa wa Singida Ramadan khoja amewashukuru na kuwapomgeza Ramadan Charity pamoja na wadau mbalimbali waliojitokeza kujitolea sadaka kwa watu wenye mahitaji Maalum katika kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Mwenyekiti Wa Taasisi ya Bustaanul a’arifiina Islamic fordeshen Rajabu Shabani amewashukuru Ramadhan Charity 2025 kwa Kuendelea kuwapati swadaka ya iftari kila mwaka na huu ni mwaka wa nne mfululizo wakitupatia swadaka hii.
“Mimi pamoja na vijana wangu tunqomba muendele kuwa na moyo huo huo wakutoa na kusaidia watu wenye huitaji katika jamii yetu na watu wengine waige Taasisi hii na wawo wewe wanatoa kwa waitaji kwani hukitoa mwenyezi mungu na kuzidishia nakuwakinga na mbala mbali mbali, towa swadaka upate Nuru kwenye maisha yako”.
Kwa upande wa vijana vituo hivyo wameshukuru na kuwapongeza Ramadhan Charity kwa kila mwaka kwa kuwapitia Iftar katika Kipindi Cha Ramadhani.
“Sisi hatuna chakulipa ila mwenyezi Mungu ndio atawalipa tutazidi kuaombea Dua kwa mwenyezi mungu,awajalie Neema na Furaha hapa Duniani”
Taasisi ya Ramadhani Charity Program 2025 imetoa sadaka Iftar ya mchele, Sukari, unga wa uji, ngano, Tambi na Tende.Taasisi hiyo inafanya harakati za kutoa misaada hii kila mwaka na mwaka huu tayari imetoa misaada kwa mikoa mitano na inaendelea kutoa hadi mwisho wa mwezi mtukufu.
Vituo vilivyo patiwa iftar Taasisi ya Bustaanul a’arifiina Islamic fordeshen, Tasisi ya manyoni,shule ya St. Agastini ya Itigi