TETE FOUNDATION kupitia mradi wake wa “TUNAAMINI KATIKA WEWE” wamekuwa wakigawa mahitaji/vifaa vya shule kwa watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu na wenye uhitaji maalumu kwa kuhakikisha mtoto hakosi shule mwaka mzima kwa sababu ya kutokuwa na mahitaji ya shule (Sare za shule, madaftari, Begi, viatu n.k)……

Mradi huu wa “Tunaamini katika wewe” unao dhaminiwa na Kampuni ya Reliance Insurance kwa takribani miaka mitatu sasa, umeongeza ufaulu wa watoto mashule na kupunguza utoro mashuleni.

Zoezi hili la ugawaji wa mahitaji ya shule ulienda sambamba na Bonanza la Michezo lililojumuisha shule za msingi na Sekondari zilizopo katika kata ya Miono lililokuwa na dhumuni la kuwaleta watoto pamoja ili kuweza kutambuana na kushirikiana kwenye masomo ili kukuza ufaulu mashuleni
Imetolewa
Afisa Habari