Ofisi ya BAKWATA Mkoa wa Singida kupitia sheikh wa Mkoa wa Singida Issa Bin Nassoro amezipongeza Ramadhani Charity Programme inayo ongozwa na Ndg. Ahmed Misanga na Taasisi ya JAI kwa kutoa sadaka Magereza ya Manispaa ya Singida.
Hayo ameyasema leo katika ziara yake ya kutembelea Wafunguwa kwenye Gereza la Manispaa ya Singida nakutoa Sadaka Iftar kwa Wafungwa kwa ajili ya kupata Futari pamoja na daku ambapo Sadaka hizo zimetolewa na Taasisi za Ramadhani Charity Program 2025 pamoja na JAI.
Sheikh Issa awaomba watu mbalimbali kuwajali watu wenye Mahitaji na Masikini nijambo ambalo linampendeza Mungu hata mitume walifanyia wema watu masikini na wenye uhitaji.
Huku upande wa Mwenyekiti wa Taasisi ya Ramadhan Charity Program 2025 Ndg Ahmed Misanga Amesema huu ndio utaratibu wao wa kila mwaka wa kutoa Sadaka ya Iftar kwa watu wenye mahitaji Hasa Magereza na Makundi Mengine ya wenye uhitaji kwa hapa tumetoa zaidi ya miaka minne ..
Hata ivyo Missanga alisisitiza kwamba watu waliopo magerezani wanahitaji huruma ya watu waliopo Uraiani ili wawe na faraja na ukaribu wa kumjua Mungu ili wanapo rudi Uraini wawe watu wemaa katika jamii wenye hofu ya Mungu
Mkuu wa Gereza Hilo SP Yusuph Athumani Amesema Amefuraishwa na Tasisi hiyo ya Ramadhan Charity chini ya Kiongozi wake Mhe. Ahmed Misanga kwa kuwapatia Sadaka ya Iftar kwani utawasaidia sana.
“Tutatuima hii Sadaka Iftar kama milivyo kusudia na tuombea kwa mungu awalipe pale mlipo toa kwa ajili ya wafugwa wote wakike na wakiume,” amesema
Lakini pia Mwenyekiti Ahmed Missanga Ramadhan Charity ametoa Tende Tambi na Ngano, kwenye Ofisi ya Sheikh Mkuu wa Mkoa Singida kwa ajili ya wahudumu wa Ofisi hiyo na Pia kwa Viongozi wa Taasisi ya JAI Mkoa wa Singida katika kipindi hichi cha Ramadhani