Mfanyakazi wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), Sawa Ngendabanka akitoa elimu kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Galanos pamoja na kuwahamasisha wanafunzi hao kujiunga na masomo ya Uhasibu watakapomaliza masomo yao ya kidato cha sita.
Afisa Masoko na Mawasiliano Mwandamizi wa NBAA, Magreth Kageya akitoa elimu kuhusu kazi zinazofanywa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Galanos iliyopo mkoani Tanga.
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Galanos wakifuatilia vipeperushi vyenye taarifa mbalimbali za NBAA.