Mbunge wa Jimbo la Chumbuni, Mh: Ussi Salum Pondeza amewajulia hali wagonjwa na wazee wasiojiweza na kuwakabidhi Iftar ikiwa ni utaratibu aliyojiwekea kila unapofika mwezi mtukufu wa Ramadhan.
Alhaj, Pondeza ametumia fursa hiyo kuwaombea dua wagonjwa na wazee hao na kuwaeleza kuwa kipindi hiki cha kumi la mwisho la Ramadhan waendelee kukithirisha kufanya ibada ili kupata msamaha kwa Allah (S.W.A).
Aidha Pondeza, ameendelea kuiyasa jamii kuwaombea dua viongozi wakuu wa nchi akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar, Alhaj, Dk. Hussein Ali Mwinyi ili waendelee kutekeleza vyema majukumu yao.
Katika hatua nyengine, Pondeza amekagua miundombinu ya maji na mradi mpya wa kisima kinachoendelea kuchimbwa shehia ya Muembe Makumbi na kukabidhi fedha taslim kwa ajili ya kuharakisha kukamilika kwa kisima hicho.
Baadhi ya wananchi wa Jimbo la Chumbuni, wamesema hatua ya Mbunge huyo ni yakupongezwa kutokana na kujitoa kwake kuwaletea maendeleo wananchi wake.
Zaidi ya siku 20 kwenye mwezi huu mtukufu wa Ramadhan, Mh: Pondeza amezitumia kuleta faraja na furaha kwa wananchi wake.